May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mfumo kudhibiti vifo vya wajawazito waja

Dk. Dorothy Gwajima, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto

Spread the love

 

WIZARA ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, inatarajia kuanzisha mfumo wa ufuatiliaji taarifa za wajawazito, ili kupunguza vifo vya kina mama na watoto. Anaripoti Jemima Samwel, DMC … (endelea).

Taarifa hiyo imetolewa leo Alhamisi tarehe 27 Mei 2021, na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Dorothy Gwajima, katika kikao chake na wataalam wa afya, kwa ajili ya kujadili maandalizi ya utengenezaji mfumo huo.

Dk. Gwajima amesema, mfumo huo utafuatilia mwenendo wa hali ya afya za wajazito, kuanzia siku ya kwanza wanapofika kliniki, hadi siku 42 baada ya kujifungua.

“Nataka muwe mnafuatilia taarifa za wajawazito na kujua maendeleo yao, toka wanapofika kituoni siku ya kwanza, mpaka baada ya kujifungua. Kwa kuwa na data za kila siku na kujua kwa namna gani wajawazito au mama baada ya kujifungua, ameweza kupata huduma zetu,” amesema Dk. Gwjaima.

Dk. Gwajima amesema mfumo huo ukianza kutumika, utasaidia wataalamu wa afya kutambua changamoto zinazowakabili wajawazito, ili kuzitafutia ufumbuzi hatimaye kuzuia vifo.

Aidha, Dk. Gwajima amewaagiza wataalam wa afya nchini, kuwa na matumizi sahihi ya takwimu za wajawazito, ili kuzihifadhi kwenye mfumo huo.

Dk. Gwajima amesema, katika kupambana na vifo vya wajawazito, Serikali imefanya mambo mengi ikiwemo kuanzisha Kampeni maalum ya Jiongenze Tuwavushe Salama, iliyoanzisshwa na Rais wa Tanzania , Samia Suluhu Hassan, yenye lengo la kupunguza vifo hivyo.

error: Content is protected !!