April 13, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mfumko wa bei washuka

Ruth Minja, Mtakwimu Mkuu wa Serikali ofisi ya Taifa ya Takwimu

Spread the love

MFUMKO  wa bei wa taifa kwa mwaka ulioishia Januari 2020, umepungua hadi asilimia 3.7 kutoka asilimia 3.8 kwa mwaka ulioishia Desemba 2019. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Kwa mujibu wa taarifa kwenye vyombo vya habari, mtakwimu mkuu wa serikali ofisi ya taifa ya Takwimu Ruth Minja amesema, kwa sasa mfumko wa bei umepungua.

Ruthi amesema, taarifa hiyo ni kutoka mwezi Januari mwaka huu ambayo ilitakiwa kutolewa 8 Februari mwaka huu.

Amesema kuwa, hali hiyo inamaanisha kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia Januari 2020, imepungua ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia Desemba 209.

Amesema, kupungua kwa mfumko wa bei kwa mwaka ulioishia Januari 2020, kumechangiwa na kupungua kwa bei za baadhi ya bidhaa za vyakula na bidhaa zisizo za vyakula kwa kipindi kilichoishia mwezi Januari 2020, zikilinganishwa na bei za Januari 2019.

Amesema, baadhi ya bidhaa za vyakula zilizopungua bei kwa Januari 2020 zikilinganishwa na bei za Januari 2019, ni pamoja na Dagaa kwa asilimia 1.4,viazi kwa asilimia 3.4, magimbi kwa asilimia 7.1 na ndizi za kupika kwa asilimia 2.8.

Na kwamba, kwa upande mwingine baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula, zilipungua bei kwa Januari 2020, zikilinganishwa na bei za Januari 2019, ni pamoja na Gesi kwa asilimia 2, mafuta ya taa kwa asilimia 4.6, Petrol kwa asilimia 1.5 , Dozeli kwa asilimia 1.3 na majiko ya gesi kwa asilimia 4.6.

Amesema, mfumko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwaka ulioishia Januari 2020, umepungua hadi asilimia 5.7 kutoka asilimia 6.3 kwa mwaka ulioishia Desemba 2019.

Hata hivyo alisema hali ya mfumko wa bei kwa nchi za Afrika Mashariki kwa mwaka ulioishia mwezi Januari 2020 kwa Nchini kenya mfumko wa Bei kwa mwaka ulioishia mwezi Januari 2020 umepungia hadi asilimia 5.78 kutoka asilimia 5.82 kwa mwaka ulioishia mwezi Disemba 2019.

Alissma kwa upande wa Nchi ya Uganda mfumko wa Bei kwa mwaka ulioishia mwezi Januari 2020 umepungua pia hadi asilimia 3.4 kutoka asilimia 3.6 kwa mwaka ulioishia  Desemba 2019.

error: Content is protected !!