Tuesday , 26 September 2023
Home Kitengo Maisha Elimu Mfuko wa Jimbo Musoma Vijijini wamwaga mamilioni ujenzi maabara za sekondari
Elimu

Mfuko wa Jimbo Musoma Vijijini wamwaga mamilioni ujenzi maabara za sekondari

Spread the love

 

MFUKO wa Jimbo la Musoma Vijijini, Mkoa wa Mara, umetoa fedha kiasi cha Sh. 75.8 milioni, kwa ajili ya ujenzi na ukamilishaji wa maabara za masomo ya sayansi kwenye shule za sekondari jimboni humo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mara … (endelea).

Taarifa hiyo imetolewa hivi karibuni na Ofisi ya Mbunge wa Musoma Vijijini, Prof. Sospeter Muhongo, ambapo imesema lengo la utolewaji fedha hizo ni jimbo hilo kuwa na shule za kidato cha tano na sita katika masomo ya sayansi, ndani ya miaka mitatu.

“Tarehe 17 Machi 2023, Mwenyekiti wa Mfuko wa Jimbo, Prof. Muhongo ameongoza kikao cha Kamati ya Mfuko wa Jimbo kilichogawa vifaa vya ujenzi vitakavyonunuliwa kwa kutumia fedha za Mfuko huo. Fedha hizo zimetunzwa na Halmashauri yetu (Musoma DC) na ndiyo itakayofanya manunuzi ya vifaa vya ujenzi,” ilisema taarifa hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, miongoni mwa vifaa vitakavyonunuliwa na fedha hizo ni mifuko ya saruji 1,613, mabati 947 na nondo 337, huku shule mpya zikipewa kipaumbele katika ugawaji wa vifaa hivyo.

Jimbo la Musoma Vijijini lenye kata 21, lina shule za sekondari 27, ambapo 25 za Serikali na mbili za madhehebu ya dini.

1 Comment

  • @THINK/Dedication/Remember”@ EMPLOY/US THEM ALL – ALL TANZANIAN HAS JOB TO DO

    In 2021, the unemployment rate in Tanzania remained nearly unchanged at around 2.74 percent. With a decline of 0.04 percentage points, there is no significant change to 2020. Over the observed period, the unemployment rate has been subject to fluctuation.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Elimu

Green Acres kuwakatia bima wanafunzi wote

Spread the loveShule ya Green Acres imejipanga kufanya mambo makubwa kwa mwaka...

Elimu

Vipaji Green Acres vyawafurahisha wazazi

Spread the love WANAFUNZI wa Shule ya Msingi Green Acres, wamewapagawisha wazazi...

ElimuHabari Mchanganyiko

Mtwara Girls waondokana na changamoto ya maji

Spread the love  WANAFUNZI wa Shule ya Sekondari ya Wasichana mkoani Mtwara...

Elimu

Rc Singida atoa siku 7 kukamilisha miradi elimu ya sekondari

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Singida Peter Selukamba ametoa siku saba...

error: Content is protected !!