Sunday , 5 February 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Mfugale wa Tanroads afariki dunia
Habari MchanganyikoTangulizi

Mfugale wa Tanroads afariki dunia

Aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), Mhandisi Patrick Mfugale
Spread the love

 

MTENDAJI Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), Mhandisi Patrick Mfugale amefariki dunia leo Jumanne, tarehe 29 Juni 2021, jijini Dodoma. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa kutoka wizara ya ujenzi na uchukuzi zinaeleza, Mhandisi Mfugale, ameugua ghafla akiwa kikaoni na kukimbizwa katika moja ya hospitali jijini humo, kwa matibabu, lakini alifikwa na mauti.

Hadi anafikwa na mauti, Mhandisi Mfugale amesimamia ujenzi wa madaraja zaidi ya 1400 nchini yakiwemo; Daraja la Mkapa Rufiji, Daraja la Umoja linalounganisha Tanzania na Msumbiji lililoko Mkoa wa Ruvuma na Daraja la Rusumo, mkoani Mara.

Mengine ni; Daraja la Kikwete huko Magarasi, mkoa wa Kigoma na Daraja la Juu la Tazara ambalo limepewa jina lake ‘Mgufale Flyover.’

Wakati wa uzinduzi wa Daraja hilo la Tazara, uliofanyika tarehe 27 Septemba 2018 ambapo Hayati Magufuli aliamua kutambua mchango wa Mfugale na kuagiza Daraja hilo liitwe ‘Mfugale Flyover.’

 

Pia, Mhandisi Mfugale amesimamia ujenzi wa, Daraja la Juu la Ubungo linaloitwa ‘Daraja la Kijazi’ pamoja na Daraja la Tanzanite, linaloendelea kujengwa Dar es Salaam na Daraja la JPM ambalo linaunganisha Kigongo- Busisi, mkoani Mwanza.

Mara ya mwisho, Mhandisi Mfugale alionekana katika shughuli ya kitaifa tarehe 14 Juni 2021, wakati Rais Samia Suluhu Hassan, alipofanya ukaguzi wa Daraja hilo la JPM, kujionea maendeleo ya ujenzi huo.

Mwaka 2018, Mhandisi Mfugale alitunukiwa tuzo ya uhandisi ya ‘Engineering Execellency.”

Mhandisi Mfugale aliajiriwa wizara ya ujenzi mwaka 1977 huku akiwa amehudumu nafasi hiyo ya juu Tanroads kwa miaka kumi na miezi sita.

Aliteuliwa kushika wadhifa huo, tarehe 23 Mei 2011 na aliyekuwa waziri wa ujenzi wa wakati huo, Dk. John Pombe Magufuli ambaye baadaye katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, Magufuli, alichaguliwa kuwa Rais wa Tanzania.

Hata hivyo, Dk. Magufuli, alifikwa na mauti, tarehe 17 Machi 2021, katika Hospitali ya Mzena, iliyopo Makumbusho mkoani Dar es Salaam na nafasi yake kuchukuliwa na Samia Suluhu Hassan.

Kabla ya uteuzi huo, Mhandisi Mfugalea alikuwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Tanroads na amewahi kushika nafasi mbalimbali katika serikali na kusimamia ujenzi wa barabara na madaraja muhimu kwa taifa.

Pia, Mhandisi Mfugale, aliwahi kushika majukumu maalumu katika wizara ya ujenzi kama Mkurugenzi wa Idara ya Barabara za Mikoa.

Mhandisi Mfugale ambaye ana Shahada ya Uhandisi kutoka Chuo Kikuu cha Roorkee India, Shahada ya Uzamili kutoka Chuo Kikuu Loughborough cha Uingereza, ni mhandisi aliyekuwa amesajiliwa na amehudhuria mafunzo ya Ujenzi na uchumi, Mafunzo ya miradi na utunzaji wa barabara pamoja na ujenzi na utunzaji wa madaraja.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Haya hapa majina 12 ya familia moja waliofariki kwenye ajali Tanga

Spread the love  MAJINA 12 kati ya 17 ya waliofariki dunia katika...

Habari Mchanganyiko

Rais Samia awalilia 17 waliofariki ajalini wakisafirisha maiti

Spread the love  RAIS Samia Suluhu Hassan, ametuma salamu za rambirambi kwa...

Habari Mchanganyiko

Wanawake wachimbaji wajenga zahanati kuokoa afya za wakazi 2000

Spread the love  ZAIDI wakazi 2,000 wa kijiji cha Nyamishiga Kata ya...

Habari Mchanganyiko

Baada ya Congo DR, Somalia mbioni kujiunga na EAC

Spread the love  TAIFA la Somalia liko mbioni kuwa mwanachama rasmi wa...

error: Content is protected !!