November 29, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mfalme wa Japan ang’atuka mwenyewe

Mfalme wa Japan, Akihito

Spread the love

MFALME wa Japan, Akihito (85) ameng’atuka katika wadhifa huo baada ya kutawala kwa miongo mitatu, kutokana na kusumbuliwa na maradhi. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Mfalme Akihito ameachia ngazi jana tarehe 30 Aprili 2019 na nafasi yake kuchukuliwa na mtoto wake, Naruhito.

Mfalme mpya, Naruhito anayetarajiwa kukasimishwa mamlaka ya ufalme leo Jumatano tarehe 1 Mei 2019, anaanza majukumu yake rasmi kwa mujibu wa katiba na sheria za Japan.  

Mfalme Naruhito wakati akiapa, aliahidi kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa katiba na sheria za taifa hilo.

Mfalme aliyemaliza muda wake, Akihito alishukuru wananchi wa Japan  na kuwahimiza kuendelea kuienzi amani.

error: Content is protected !!