September 25, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mfahamu Kanali aliyemng’oa Rais wa Guinea

Spread the love

 

MAMADY Doumbouya, Kanali kiboko aliyemmaliza utawala wa Rais wa Guinea, Alpha Conde amepata mafunzo ya kivita katika nchini za Israel, Ufaransa. Anaripoti Gabriel Mushi … (endelea).

Tarehe 5 Septemba 2021, , nchi ya Gunea iliandika historia nyingine baada ya kutokea mapinduzi ya kushtukiza ambayo yamefanikiwa kumuondoa madaraka Rais Alpha Conde.

Mapinduzi hayo yaliyofanywa na kikosi maalumu cha wanajeshi maarufu kama (GFS), yamesitisha ndoto za Conde kusalia madarakani kwa awamu ya tatu ungwe ambayo ameitumikia kwa mwaka mmoja pekee baada ya uchaguzi mkuu kufanyika Oktoba 2020.

Conde mwenye umri wa miaka 83, alizuiliwa na wanajeshi wa kikosi hicho cha GFS, kwa saa kadhaa baada ya kuripotiwa kwa ufyatulianaji wa risasi karibu na makazi ya rais yaliyopo katika jiji la Conakry nchini Guinea.

Fuatilia simulizi hii ya Kanali Doumbouya kupitia Video hii ili kuweza kumjua kwa undani zaidi.

error: Content is protected !!