Tuesday , 5 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa ‘Meya’ Ubungo atimkia ACT-Wazalendo
Habari za SiasaTangulizi

‘Meya’ Ubungo atimkia ACT-Wazalendo

Ramadhan Kwangaya
Spread the love

RAMADHANI Kwangaya, aliyekuwa Kaimu Meya wa Manispaa ya Ubungo jijini Dar es Salaam amejiunga na chama cha ACT-Wazalendo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Kwanganya ambaye alikuwa Diwani wa Manzese kupitia Chama Cha Wananchi (CUF) amechukua uamuzi huo siku chache kupita tangu Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Ubungo kuvunjwa.

Taarifa iliyotolewa leo Jumatano tarehe 17 Juni 2020 na Naibu Katibu wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma wa ACT-Wazalendo, Janeth Rithe imesema, Kwanganya amejiunga na chama hicho pamoja na aliyekuwa Diwani wa Viti Maalum (CUF) Manispaa ya Ubungo na Diwani wa Jiji la Dar es Salaam, Leila Madibi.

Kwangaya ambaye alikuwa Naibu Meya wa Manispaa ya Ubungo alikaimu nafasi ya Meya wa Ubungo kuanzia tarehe 12 Mei 2020 baada ya Boniface Jacob kupoteza sifa za kuwa Meya.

Jacob ambaye pia alikuwa Diwani wa Ubungo alipoteza nafasi ya umeya baada ya barua inayoelezwa kuandikwa tarehe 28 Aprili 2020 na katibu wa Chadema Kata ya Ubungo kwenda kwa mkurugenzi wa halmashauri ya Ubungo kuonyesha amevuliwa uanachama hivyo kupoteza sifa za kuwa meya.

Hata hivyo, Jacob mwenyewe, Chadema makao makuu na mtu huyo ambaye jina lake lilitumika kwenye barua hiyo kudai haina ukweli, kwani hakuna kikao chochote kilichokaa cha kumjadili Jacob kisha kumvua uanachama.

Jacob alifikisha suala hilo Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) kuonyesha kutokubaliana na uamuzi wa mkurugenzi wa Ubungo.

Hadi sasa, hakuna kilichoelezwa juu ya rufaa hiyo iliishia wapi kwani si Tamisemi au Jacob waliozungumzia suala hilo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Dk. Biteko: Viongozi tuache alama nzuri katika utendaji wetu

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaTangulizi

Chanzo maporomoko yaliyoua 65 Hanang, chatajwa

Spread the loveSERIKALI imesema kumeguka kwa sehemu ya Mlima Hanang ambao ilikuwa...

Habari za Siasa

Baba yake Ole Sabaya ashinda Uenyekiti CCM – Arusha

Spread the loveLoy Thomas Sabaya ambaye ni Baba wa aliyekuwa Mkuu wa...

Habari za Siasa

Serikali yaagiza uchunguzi chanzo maporomoko Hanang

Spread the loveSERIKALI imeagiza uchunguzi ufanyike ili kubaini chanzo cha maporomoko ya...

error: Content is protected !!