March 7, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Meya Mwanza akamatwa asimwage mboga mbele ya Rais Magufuli

Meya wa Jiji la Mwanza, James Bwire. Picha ndogo, Kiomoni Kibamba, Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza

Spread the love

MEYA wa Jiji la Mwanza, James Bwire amekamatwa na jeshi la Polisi muda mchache kabla ya kutoa salamu zake kwa Rais John Magufuli katika uzinduzi wa kiwanda cha Sayona kwa kuhofia kutoa siri ya ufisadiwa ujenzi wa kiwanda hicho, anaandika Mwandishi Wetu.

Tukio hilo limetokea baada ya kubainika katika salamu za Meya kwa Rais Magufuli, kulikuwa na maelezo ya ufisadi wa kiwanda hicho kilichopo Nyakato Ilemela jijini Mwanza.

Wanaotajwa kufanya ufisadi huo ni mkurugenzi wa Jiji hilo, Kiomoni Kibamba na viongozi wengine wa mkoa huo.

Pia viwanda vya kampuni hiyo vimekuwa vikituhumiwa kuwanyanyasa wafanyakazi wake wengine wakitimuliwa kazi bila kulipwa stahiki zao.

Baada ya kamati ya Ulinzi na usalama mkoa wa Mwanza chini ya John Mongella kubaini kwamba Meya huyo anataka kumwaga ukweli mbele ya rais, inadaiwa aliliagiza jeshi la Polisi kumkamata kiongozi huyo ambaye kwa kipindi kifupi ameonekana akifichua uchafu unaofanyika katika jiji la Mwanza.

error: Content is protected !!