August 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Meya Mpanda azimwagia sifa Wizara, Tume Madini

Spread the love

MEYA wa Mpanda, Haidary Hemed ameipongeza Wizara ya Madini kwa uanzishwaji wa masoko ya madini nchini ambayo yamekuwa mkombozi wa wachimbaji wadogo wa madini huku serikali ikikusanya mapato. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mbeya … (endelea).

Kutokana na hali hiyo Hemed amesema Sekta ya Madini imekuwa na mchango mkubwa kwenye Pato la Taifa.

Ametoa pongezi hizo leo Jumatano tarehe 3 Agosti, 2022, mara baada ya kutembelea banda la Tume ya Madini katika Maonesho ya Nane Nane yanayofanyika Kitaifa katika Viwanja vya John Mwakangale Mkoani Mbeya.

“Soko la Madini la Mpanda linafanya vizuri sana, napongeza kazi kubwa inayofanywa na Waziri wa Madini Dk. Doto Biteko ya usimamizi wa masoko kupitia Tume ya Madini.” amesema Hemed.

Katika hatua nyingine, amepongeza kasi ya utoaji wa leseni za madini inayofanywa na Tume ya Madini na kuongeza kuwa tangu uanzishwaji wa Tume, wachimbaji wengi wa madini wameendelea kupata leseni na kuchimba madini hivyo kuongeza mapato yanayotokana na Sekta ya Madini.

error: Content is protected !!