Friday , 1 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Meya Mbeya: Ushiriki wanasiasa, wananchi unahitajika
Habari za Siasa

Meya Mbeya: Ushiriki wanasiasa, wananchi unahitajika

David Mwashilindi, Mstahiki Meya wa Jiji la Mbeya (Chadema)
Spread the love

DAVID Mwashilindi, Mstahiki Meya wa Jiji la Mbeya (Chadema) amesema, katika kuhakikisha maendeleo yanawafikia wananchi, kunahitajika uwajibikaji wa pamoja kati ya wanasiasa na watumishi wa umma. Anaripoti Danson Kaijage, Da es Salaam…(endelea).

Mwashilindi ametoa kauli hiyo leo tarehe 19 Februari 2020, alipozungumza na waandishi wa habari jijini humo kuhusu mafanikio yaliyopatikana katika Jiji la Mbeya kwa kipindi cha miaka mitano sasa.

Amesema, Jiji la Mbeya limeweza kufanya shughuli za kuwapatia wananchi maendeleo kutokana na baraza la halmashauri ya jiji hilo, kwa kushirikiana vyema na watumishi wa umma kwa kila mmoja kisimamia majukumu yake.

Aidha ameeleza, kuwepo kwa vyama vya siasa ambavyo havifanani kwa mitazamo, kwamba haiwezi kuwa sababu ya kuzuia au kufanya maendeleo kuzorota.

Katika hatua nyingine Meya Mwashilindi amesema, kwa sasa Jiji la Mbeya limekuwa jiji la kwanza katika kujenga shule zenye mchepuo wa Lugha ya Kiingereza n ahata Waziri wa Tamisemi, Seleman Jafo kulipigia mfano.

Pamoja na kuwepo kwa shule za mchepuo wa Kiingereza amesema, kwa sasa Jiji la Mbeya limekuwa na urahisi wa kuingia na kutoka, kwani miundombinu hiyo imewezesha kuondokana na msongamano ambao ulikuwepo hapo awali.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Mwili wa Hayati Mwinyi kuagwa leo saa 8 Uwanja wa Uhuru

Spread the loveMWILI wa Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi unatarajiwa kuagwa kuanza...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Mwinyi kuzikwa Machi 2 visiwani Unguja

Spread the loveMWILI wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Pili wa Tanzania,...

Habari za SiasaTangulizi

Rais mstaafu Mwinyi afariki dunia

Spread the loveRais Mstaafu wa awamu ya pili wa Tanzania, Ally Hassan...

Habari za Siasa

Waziri mkuu Ethiopia atua Tanzania

Spread the loveWaziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Shirikisho la Ethiopia,...

error: Content is protected !!