August 17, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Meya Kafana: Wapuuzeni wanaotaka kutuchafua

Spread the love

MUSA Kafana, Naibu Meya wa Jiji la Dar es Salaam amewataka wananchi kupuuza taarifa zinazosambazwa kupitia mitandao ya kijamii kwamba jiji hilo limetoa tenda ya ukusanyaji wa ushuru wa maegesho kwa wazabuni wasiokuwa na vigenzo, anaandika Mwandishi Wetu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo ofisini kwake Kafana amesema, Jiji haliwezi kufanya mzaha na makusanyo ya fedha za wananchi kwa kumpa mzabuni asiyekidhi vigezo.

“Ni kweli tulitangaza tenda hiyo na kupata wazabuni watatu ambao walikidhi vigenzo vya awali, wazabuni hao walichaguliwa kati ya kampuni nyingi zilizokuwa zimeomba ikiwemo Kenya Airport (KAPS), kwa upande wa Manispaa ya Ilala ambao waliahidi kukusanya Sh. 54 bilinioni za Tanzania kwa mwaka huku wakitakiwa kuweka bondi ya Sh. 5.4 bilioni kabla ya kuanza kazi,” amesema.

Kafana amewataja wazabuni wengine kuwa ni UBAPA ambao waliahidi kukusanya Sh. 115.13 bilioni kwa mwaka katika Manispaa ya Kinondoni ambao pia waliahidi kuweka bondi ya Sh. 1.51 bilioni, CHEPAUTWA walioahidi kukusanya Sh. 5.64 bilioni kwa mwaka katika Manispaa ya Temeke, waliosaini bondi ya Sh. 564 milioni.

Kafana ambaye ni diwani wa kata ya Kiwalani kupitia Chama Cha Wananchi (CUF), anasema kati ya wazabuni hao watatu ni mmoja tu ambaye hajatimiza vigezo na bado hajaanza kazi huku wengine wakiendelea.

“Mzabuni ambaye hajatimiza vigezo ni KAPS, wao hawajasaini bondi waliyotakiwa kuleta, hawana barua ya usajili na kutambuliwa kisheria. Kwa kuwa huu ulikuwa ni mchakato basi tunangalia namna ya kuwaondoa na kuwapa wengine lakini si kweli kwamba tumewapa tenda hii,” amesema Kafana.

“Ieleweke kwamba, sio kwamba wazabuni waliokuwepo mwanzo hawaleti fedha ama wamekiuka makubaliano ila tunaangalia kiwango cha fedha ambacho wazabuni wapya waliahidi kuleta. Lengo kubwa ni kupata fedha ili ziwasaidie wananchi,” amesema.

Kafana amebainisha kuwa hadi kufikia wiki ijayo Jiji la Dar es Salaam litakuwa limeshapata mzabuni mpya ambaye atakuwa amekidhi vigezo.

error: Content is protected !!