Tuesday , 27 February 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Meya Ilala ‘kazi kazi’
Habari za Siasa

Meya Ilala ‘kazi kazi’

Charles Kuyeko, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala
Spread the love

CHARLES Kuyeko, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala amefanya ziara ya kikazi katika kata ya Tabata mtaa wa tabata Kisiwani na matumbi, anaandika Mwandishi Wetu.

Kuyeko amefanya ziara hiyo akiambatana na Msongela Palela, Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala huku Patrick Asenga, diwani wa Kata hiyo na Christopher Victor mwenyekiti wa mtaa wa Tabata Kisiwani wakiwa ni wenyeji wao.

Ziara hiyo imelenga kukagua ubora wa daraja la Mwananchi, na athari za mto Tenge na mto Luhanga kwa wakazi wa maeneo hayo.

Akizungumza kwa niaba ya wananchi wa mtaa wa Tabata Kisiwani Victor, mwenyekiti wa serikali ya mtaa huo amesema mto huo ni kero kubwa kwa wananchi kutokana na daraja la Mwananchi kutouwa na ubora kuweza kupitisha maji kwa kiwango kinachotakiwa.

“Mvua zinaponyesha maji yanakuja kwa wingi na uchafu mwingi unaziba njia za daraja hilo kwani lipo chini sana na pia njia/chemba zake ni ndogo zinashindwa kupitisha uchafu na hapo ndipo maji hulazimika kutafuta njia katika makazi ya watu,” amesema.

Kwa upande wake Assenga, diwani wa kata hiyo amesema “mito imezibwa na baadhi ya matajiri waliojenga katika kingo za mto  na kujajaza vifusi katika kingo za mito, na kushindwa kupitisha maji.

“Kwa bahati nzuri mhandisi wetu wa Manispaa yuko hapa, naomba kwa niaba ya wananchi wangu kero hii ichukuliwe na kutatuliwa kwa njia ya dharura kwani mvua zikinyesha eneo hili ni hatari kwa wananchi.”

Akitolea majibu tatizo hilo, Kuyeko amemtaka mkurugenzi wa manispaa ya Ilala kufanya mazungumzo na mkurugenzi wa manispaa ya Ubungo kwani mto huo upo mpakani ili waweze kutafutia ufumbuzi jambo hilo na ikibidi kutenga bajeti ya pamoja kwa ajili ya kujenga daraja lenye ubora.

“Mkandarasi wa manispaa ya Ilala alete wataalamu katika eneo hili ili wafanye utatuzi wa awali ikiwemo kusafisha mito hiyo hususan na kufungua njia zote za majina kwamba kama kuna matajiri waliojenga katika njia za mto huo basi sheria ifuate mkondo wake,” amesema.

Meya Kuyeko pia amemtaka afisa mazingira wa Ilala kufanya mawasiliano ya haraka na NEMC ili iweze kushughulika na wavamizi wa mto huo kwani maji ya mto huo ni machafu sana na huenda kuna kemikali zinatirrishwa katika mto Luhanga.

Msongela Palela, mkurugenzi wa manispaa hiyo ameahidi kutekeleza kutuma wataalamu kwa haraka kutokana ili kulitafutia ufumbuzi tatizo linalowakumba wananchi hao.

Akitoa maoni yake baada ya ziara hiyo, Brown Mwakalikamo mmoja kati ya wananchi wa mtaa wa Kisiwani amesema, “sisi wananchi wa Tabata Kisiwani na Matumbi tumepata matumaini mapya na tunaimani kubwa sana na wewe Meya maana taarifa zako tunazo kuwa wewe ni mzee wa vitendo.”

Amempongeza pia, diwani Patrick Assenga wa kata hiyo kwa kuguswa na kero hiyo na kusimama upande wa wananchi katika kuitafutia ufumbuzi kero hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Hamahama Ngorongoro kutikisa maandamano ya Chadema Arusha

Spread the loveMAELFU ya wanachama na wafuasi wa Chama cha Demokrasia na...

Habari za SiasaTangulizi

Waliofariki ajalini Arusha kuagwa siku ya maandamano Chadema

Spread the loveMIILI ya watu 25 waliofariki dunia katika ajali iliyohusisha lori...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali kuiburuzwa mahakamani ajali iliyoua 25 Arusha

Spread the loveMTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), imeitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Samia atoa pole ajali iliyoua 25, kujeruhi 21 Arusha

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za rambirambi kwa Mkuu...

error: Content is protected !!