June 19, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Meya Ilala awajulia hali Dk. Masaburi, Mhere Mwita

Spread the love

CHARLES Kuyeko, Mstahiki Meya wa  Manispaa ya Ilala, jijini Dar es Salaam amefika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili asubuhi ya leo na kuwatembelea wanasiasa Dk. Didas Masaburi na Mhere Mwita waliolazwa hospitalini hapo, anaandika Faki Sosi.

Dk. Masaburi ambaye aliwahi kuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam na aligombea ubunge Jimbo la Ubungo katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana, amelazwa katika Hospitali ya Muhimbili kutokana na ugonjwa ambao mpaka sasa bado haujawekwa wazi.

Mbali na kumjulia hali Dk. Masaburi, Meya huyo pia amemtembelea Mwita Mhere, Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha), Mkoa wa Geita, ambaye alipata ajali wiki iliyopita mkoani Dodoma.

Mhere amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili katika Kitengo cha Mifupa (MOI), akitibiwa majeraha yaliyotokana na ajali hiyo ambapo mchana wa leo ameripotiwa kuzidiwa na kupelekwa katika chumba cha wagonjwa mahututi yaani ICU.

Kuyeko amewapa pole wagonjwa hao na kusema, anawaombea kwa Mungu ili awaponye haraka na warejee kwenye majukumu yao ya kawaida ili waendelee kulijenga taifa.

error: Content is protected !!