August 17, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Meya: Huduma za afya nchini zimezorota

Spread the love

UPUNGUFU wa watumishi katika Sekta ya Afya nchini, umetajwa kuzorotesha huduma za afya katika hospitali, vituo vya afya na zahanati mbalimbali zinazomilikiwa na serikali, anaandika Pendo Omary.

Akizungumza na MwanaHALISI Online, Charles Kuyeko, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala amesema mahitaji ya madaktari bigwa katika hospitali mbili za serikali zilizopo katika manispaa hiyo ni madaktari 23, wakati waliopo kwa sasa ni madaktari 11 hivyo madaktari 12 bado wanahitajika.

“Kwa upande wa madaktari wa kawaida mahitaji ni madatari 327 wakati waliopo ni madaktari 272 hivyo bado madaktari 55 wanahitajika.

“Maafisa wauguzi na maafisa wengine wanaohitajika ni 505 waliopo ni maafisa 431 hivyo bado maafisa 74 wanahitajika,” amesema Kuyeko.

Kuhusu wauguzi amesema katika manispaa hiyo, wanahitajika wauguzi 400 wakati waliopo ni wauguzi 379 hivyo 21 wanahitajika.

Pia kwa upande wa maafsa afya na maafisa afya wasaidizi wanaohitajika ni 113 ambapo waliopo ni 109.

“Wahudumu wa afya, watunza kumbukumbu na watumishi wengine wanaohitajika ni 299 lakini kwa sasa wapo 281 hivyo bado wahudumu 18 wanahitajika. Upungufu huu umekuwa ukikwamisha huduma bora kwa wananchi,” ameeleza Kuyeko.

Hata hivyo malengo ya mpango wa mwaka 2015/2016-2020 katika seta hiyo kwa upande wa manispaa ya Ilala yanajumuisha ujenzi wa hospitali 1, vituo vya afya viwili, zahanati tano, nyumba za watumishi wa afya 10  na kuwa na vituo vya ushauri nasaha (AIDS/HIV) 40.

 

error: Content is protected !!