January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Meya cup Mwanza kutimua vumbi Julai 19

Michuano ya Pepsi Kombe la Meya CUP Mwanza mwaka jana

Spread the love

MICHUANO ya kuwania Kombe la Meya wa Jiji la Mwanza (Meya  Cup 2015), utepe wake utakatwa Julai 19 mwaka huu. Anaandika  Moses Mseti, Mwanza … (endelea).

Aidha, katika ufunguzi huo kutakuwa na  mchezo kati ya Bingwa Mkolani na washindi wa pili wa michuano hiyo mwaka jana, kombaini ya Kata ya  Isamilo. 

Mechi hiyo itafanyika  kwenye uwanja wa Nyegezi  Jeshini, itatanguliwa na mchezo  kati ya kombaini ya wachezaji wakongwe mbalimbali na MwanzaStarehe veterani.

Mwasisi wa michuano hiyo aliyekuwa Meya wa Jiji la Mwanza, Stanslaus Mabula, amesema zawadi zake zimeboreshwa tofauti na ilivyoanza. 

Amesema udhamini wa mwaka huu mbali na zawadi, umeongezeka kutoka sh.75 milioni hadi  sh.90 milioni, ongezeko ambalo limelenga kuwasaidia na kuwakwamua wachezaji kwa kuwa na kitega uchumi,waweze kuendesha maisha yao.

“Tulibuni kitu cha kuwakutanisha wanamichezo, mpango wa kwanza ulikuwa ni mpira wa miguu licha ya changamoto ya udhamini,nawashukuru Pepsi kwa kukubali kudhamini mashindano haya kwa mkataba wa miaka mitatu na leo tunendelea,” amesema Mabula. 

Meneja Masoko wa Pepsi Kanda ya Ziwa,Promod Nair, alisema udhamini wao ni kuunga mkono juhudi za Mabula katika kuinua na kuboresha michezo katika jiji la Mwanza na Tanzania kwa ujumla.

Awali Meneja Mauzo wa kampuni hiyo Kanda ya Ziwa, Hussein Mkwawa, amesema mashindano ya kuwania kombe la Meya licha ya kuanzia Mwanza, yametanuka ambapo mwaka jana yalichezwa katika mikoa ya Mbeya na Dodoma, mwaka huu yameanzia Shinyanga nabaadaye Mwanza na Arusha.

“Mwaka huu Pepsi tumekuja na yafuatayo,udhamini umefikia sh 130 milioni kwa Mwanza na Shinyanga. Shinyanga walipata sh. 40 milioni ni kiasi kilichobaki ni kwa ajili ya mkoa wa Mwanza,” amesema Mkwawa.

Amesema mbali na fedha,watatoa zawadi ya bingwa, pikipiki ya magurudumu matatu ya kubeba abiria, yenye thamani ya sh. 6.9, mshindi wa pili pikipiki yanye thamani ya sh.2 milioni, mipira 48, soksi jozi 408, seti 24 za jezi kwa timu zote zitakazoshiriki michuano ya mwaka huu, vikombe  na medali, kiatu cha dhahabu na vifaa vya waamuzi.

Michuano hiyo ya kombe la Meya itaanza Julai 19, mwaka huu na kufikia tamati Septemba 12, mwaka huu,yatazinduliwa kwenye uwanja wa Nyegezi na Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo,ambapo timu zote shiriki zitakuwepo, kwa ajili ya kukabidhiwa vifaa. 

error: Content is protected !!