Tuesday , 16 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa ‘Meya’ Chadema ashinda kura za maoni Moshi Mjini
Habari za Siasa

‘Meya’ Chadema ashinda kura za maoni Moshi Mjini

Aliyekuwa Meya Manispaa ya Moshi, Raymond Mboya akizungumza kwenye mkutano mkuu wa uchaguzi jimbo la Moshi Mjini baada ya kushinda kura za maoni za kugombea ubunge wa jimbo hilo.
Spread the love

ALIYEKUWA Meya wa Manispaa ya Moshi Mkoa wa Kilimanjaro, Raymond Mboya ameshinda kura za maoni za kuwania nafasi ya ubunge  kupitia Cham cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) jimbo la Moshi Mjini. Anaripoti Mwandishi Wetu, Moshi…(endelea).

Mboya ameibuka na ushindi huo leo Alhamisi tarehe 16 Julai 2020 baada ya kupigiwa kura za maoni 117 sawa na asilimia 70.9 ya kura zote 165.

Miongoni mwa washindani wake wa karibu, Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Kilimanjaro, Michael Kilawila ameoafa kura 32 sawa na asilimia 19.4, Colins Tamimu kura 10 sawa na asilimia 6 na Antony Ndewawio kura 6 sawa asilimia 3.6.

Matokeo hayo yametangazwa na msimamizi wa uchaguzi jimbo la Moshi mjini, Ephata Nanyaro ambapo amesema matokeo hayo ni mchakato wa  awali mpaka hapo halmashauri kuu itakapokaa huku akiwataka wananchi kuendea kuwa na utulivu.

“Haya ni  mtokeo ya awali na kamati kuu itakuwa na mamlaka ya mwisho na kufanya uteuzi wa mwisho,” amesema Nanyaro

Akizungumza  baada  ya matokeo hayo, Mboya amewashukuru wajumbe kwa kumuamini na kuona anaweza kusimama katika jimbo hilo ambapo amesema atakilinda chama hicho na kuhakikisha anawavusha katika uchaguzi mkuu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Samia arejesha mikopo ya 10%, bilioni 227.96 zatengwa

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amerejesha utaratibu wa utoaji mikopo...

Habari za Siasa

Rais Samia amfariji mjane wa Musa Abdulrahman

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan leo Jumanne amempa pole Mwanakheri Mussa...

Habari za Siasa

Nape: Wanasiasa, wanahabari, wafanyabiashara mteteeni Samia

Spread the loveWaziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano,...

Habari za Siasa

CAG: TAWA imegawa vibali vya uwindaji bila idhini ya waziri

Spread the loveRIPOTI ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali...

error: Content is protected !!