July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

METL yamalizana na wafanyakazi wake

Spread the love

UONGOZI wa kampuni ya Mohamed Enterprises LTD inayomiliki kiwanda cha Oil & Fats Limited kilichopo Kurasini umelaumu uongozi wa chama cha wafanyakazi, TUICO kushindwa kusimamia mgogoro kati wa fanyakazi na kampuni. Anaandika Hamisi Mguta … (endelea).

Mgogoro huo uliosababisha kuwepo kwa mgomo wa wafanyakazi juzi, Desemba 8 mwaka huu asubuhi wakiishinikiza kampuni kumfukuza Afisa rasilimali watu Erick Bubelwa kwa tuhuma za kutowatumikia wafanyakazi ipasavyo.

Baada ya Mwanahalisi Online kufika katika kiwanda hicho siku ya hiyo baada iliyotokea mgomo, imeelezwa na baadhi ya wafanyakazi kuwa sambambamba na wafanyakazi hao kushinikiza kuondoka kwa afisa huyo, matatizo kama ucheleweshwaji wa mishahara na kubanwa kwa kimaslahi katika malipo.

Mwenyekiti wa chama cha wafanyakazi, TUICO, Daudi Issa amelieleza Mwanahalisi Online kuwa malalamiko juu ya afisa huyo kuwa astahili kuwa kiongozi kutokana kwa maadili, yaliwafikia viongozi wa chama hiko mnamo tarehe 6, siku ya ijumaa ambapo uongozi wa kampuni uliutaka chama hiko kuwasilisha vithibitisho siku ya tarehe 8.

Ameeleza kuwa siku hiyo ya tarehe 8 ilipofika, ambapo wlikuwa wakijiandaa kuwasilisha vithibitisho hivyo wafanyakazi waligoma kufanyakazi kwa takribani masaa manne na kusababisha shughuli za uzalishaji kusimama kwa muda.

error: Content is protected !!