September 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

MET: Kuna haja kuboresha elimu nchini

Wanafunzi wakiwa darasani

Spread the love

MTANDAO wa Elimu Tanzania (MET), unaojumuisha asasi za kiraia 210 umeeleza, kuna haja ya kuboresha elimu nchini kwa lengo la kupata wasomi makini. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Akizungumza Jijini Dodoma leo tarehe 11 Desemba 2019, Ochola Wayaga ambaye ni Mratibu wa Taifa wa Mtandao wa Ten/Met, katika ufunguzi wa Mkutano wa 11 wa mwaka wa wadau  wa elimu nchini amesema, licha ya kuwepo juhudi kwa serikali kuboresha elimu, bado kunatakiwa uboreshaji wa miundombinu.

Wayaga amesema, ili kupata wasomi wazuri ni lazima kuangangalia ubora wa elimu katika shule za msingi na sekondari, na si kuangalia wingi wa wanafunzi waliopoma shuleni.

Na kwamba, suala la ubora wa elimu ni muhimu kwa taifa, kwani kama wanafunzi watakuwa na elimu ambayo si bora, ni wazi kuwa taifa halitaweza kuwa na maendeleo yanayokusudiwa.

Akifungua Mkutano wa Mtandao wa Ten/Met, Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk. Leonard Akwilapo amepongeza mchango wa Mtandao wa Elimu Tanzania, katika kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya elimu nchini.

Dk Akwilapo amesema, kutokana na mchango wa mtandao huo, serikali inasubiri mapendekezo kutoka kwa mkutano huo wa siku tatu ili kufanyia kazi changamoto ambazo zitakuwa zimeibuliwa na wadau wa elimu katika kuboresha zaidi elimu nchini.

Ofisa Miradi wa Mtandao wa Ten/Met, Nicodemus Shauri amesema,  serikali imefanya jitihada kubwa katika kuboresha elimu kwa kupandisha ufaulu katika matokeo ya darasa la saba na sekondari, lakini bado ufaulu upo chini katika masomo ya Kiswahili na Hesabu.

“Mkutano huo umeitishwa ili kuangalia ubora wa elimu wa  kufaulu tu katika ngazi ya msingi na sekondari, bali katika ngazi zote hadi chuo kikuu ili kutoa mapendekezo serikali ya kuboresha elimu” amesema.

Akizungumza Ofisa Mradi wa Shirika la Sense International Tanzania, Benjamini Kihwele amesema, watu wenye ulemavu mchanganyiko wanatakiwa kupewa msaada wa kuwa na wasaidizi madarasani ili kupata elimu shirikishi kikamilifu.

error: Content is protected !!