LIONEL Messi, nahodha wa Bacelona na Sergio Ramos wa Real Madri ndio vinara wa kuongoza mgomo kupinga La Liga kuchezwa Marekani. Anaandika Kelvin Mwaipungu … (endelea).
Bodi ya ligi ya La Liga ilieleza kuwa, baadhi ya mechi zitalazimika kuchezwa nchini Marekani.
Lionel Messi, anaripotiwa kuwa tayari kuongoza mgomo wa kupinga uamuzi wa mechi moja ya La Liga kuchezwa nchini Marekani kuanzia mapema msimu huu kutokana na makubaliano ya miaka 15 waliyoyafikia na kampuni ya michezo na burudani ya Relevant.
Relevant ni kampuni ambayo inaendesha mashindano ya Kombe la Kimataifa kwa ajili ya timu kujiandaa na msimu.
Taarifa kutoka Shirika la Habari la Hispania (AS) siku mbili zilizopita liliripoti kuwa baadhi ya wachezaji wa ligi hiyo wanalalamikia kutoshirikishwa katika uamuzi huo.
Wanatajwa manahodha 19 wanaoandaa mgomo dhidi ya uamuzi huo akiwemo Messi, Ramos no huo, Diego Godin wa Atletico Madrid.
Tayari manahidha hao wamekutana kuzungumzia uamuzi wa bodi hiyo.
Leave a comment