Thursday , 30 March 2023
Home Kitengo Michezo Messi, Neymar kukutana fainali, Copa America
Michezo

Messi, Neymar kukutana fainali, Copa America

Spread the love

 

FAINALI ya michuano ya Copa America, itapigwa siku ya Jumapili ambapo itaikutanisha miamba ya soka barani humo, tumu ya Taifa ya Argentina dhidi ya Brazil. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Mchezo huo ambao utapigwa siku ya Jumapili, utakwenda kushuhudia mastaa wawili wa timu hizo, Lionel Mess, pamoja na Neymar Do Santos, wakipigania kutwaa taji hilo, ambao walicheza pamoja ndani ya klabu ya FC Barcelona.

Wachezaji hao wawili walicheza kwa pamoja misimu mine kuanzia 2013/17, wakiwa ndani ya kikosi cha Barcelona na kuchukua jumla ya mataji saba na baadae Neymal kuamua kutimkia Psg ya Ufaransa.

Argentina inaongozwa na Messi imetinga fainali mara baada ya kuiondosha Colombia, kwenye hatua ya nusu fainali kwa mikwaju ya penati 3-2, mara baada ya kumaliza dakika 90, wakitoka sare ya bao 1-1.

Kwa upande wa Brazil walitinga hatua ya fainali mara baada ya kuifunga timu ya Taifa ya Peru, kwa bao 1-0.

Katika michuano hiyo lionel Messi ndio kinara kwa ufungaji, akiwa na mabao manne, na Neymal akishika nafasi ya tano kwenye idadi ya wafungaji wa michuano hiyo, akiwa na mabao 2.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

TANROADS wawataka watumishi wazingatie michezo kazini

Spread the love  WAKALA wa barabara Tanzania (TANROADS) imesema michezo inapaswa kuzingatiwa...

Michezo

Yanga: Fedha za Rais Samia zinaleta ari kubwa

Spread the loveUONGOZI wa klabu ya Yanga, umesema fedha zinazotolewa na Rais...

Michezo

Simba Sc. yamvulia kofia Rais Samia, yamuahidi makubwa dhidi ya Horoya

Spread the loveWAKATI timu ya Simba ikiibuka na ushindi wa bao 3-0...

Michezo

Taasisi ya TKO na TFF yawapiga msasa makocha wa kike 54

Spread the love WAKATI Soka la wasichana likichipua kwa kasi Taasisi ya...

error: Content is protected !!