Saturday , 4 February 2023
Home Kitengo Michezo Messi atokwa machozi, akiaga Barcelona
MichezoTangulizi

Messi atokwa machozi, akiaga Barcelona

Spread the love

 

MARA baada ya kucheza kwa miaka 21, hatimaye mchezaji hatari kwa sasa Duniani, Lionel Messi ameiaga rasmi klabu yake ya Barcelona, Uwanjani Camp Nou, kwenye mkutano wake na wanahabari.

Tukio hilo ambalo liliudhuliwa pia na wachezaji wenzake wa Barcelona, Messi alisimama mbele kwa dakika moja kabla ya kuanza kuongea na kisha kutokwa machozi, huku wenzie wakimpigia makofi.

Mchezaji huyo alisema kuwa hana neno zaidi ya Ahasante, kwa kuwa klabu hiyo imefanya kutimiza ndoto zake.

“Sina neno zaidi, ahsanteni na kwaherini nyote, Barcelona ilifanya ndoto yangu itimie” alisema mchezaji huyo huku akiwa kwenye hali ya simanzi.

Messi aliendelea kwa kusema kuwa alipaswa kubaki klabuni hapo kwa kuwa ni nyumbani, kusema kwaheri ni neno gumu.

“Nilitamani kubaki hapa, hapa ni nyumbani, nyumbani kwetu sote, mpango ulikuwa ni kubaki ila leo napaswa kusema kwaheri, kusema neno hilo ni gumu, kwa kuwa ndio klabu niliyochezea kwa maisha yangu yote.” Alinena mchezaji huyo.

Messi ameondoka ndani ya klabu ya Barcelona kutokana na vizuizi vya kifedha na utawala vilivyowekwa na La Liga licha ya kuwa tayari kusaini mkataba mpya na timu yake hiyo kama taarifa ya klabu hiyo ilivyoeleza.

“Licha ya FC Barcelona na Lionel Messi kufikia makubaliano na nia ya wazi ya pande zote mbili kutia saini mkataba mpya leo, hii haiwezi kutokea kwa sababu ya vizuizi vya kifedha na kiutawala (kanuni za Ligi Kuu ya Hispania, La Liga),” klabu imesema.

“FC Barcelona inatoa shukrani za kipekee kwa mchezaji huyo kwa mchango wake katika kukuza klabu na inamtakia kila la kheri katika siku zijazo kwenye maisha yake ya binafsi ya soka.” Imeongezeka taarifa ya Barcelona.

Katika kipindi chote akiwa ndani ya klabu hiyo Messi ameshinda jumla ya mataji 35, na kupachika mabao 672 katika mashindano yote na kuweka rekodi ya kuwa mfungaji wa muda wote ndani ya klabu hiyo.

 

 

 

 

1 Comment

  • Alitakiwa aondoke ndani ya miaka miwili baada ya Neymar Jr. kuwasili. Lakini hakuondoka…sijui kama alihonga kundelea kukaa hapo.
    Barcelona FC haijashinda sana tangu Neymar Jr aondoke.
    Ameshakimbia kilometa nyingi, na mpira wa kisasa hauhitaji wachezaji wa Kati wacheze kwa ajili yake.
    Tuone kama ataweza huko aendako.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Vigogo wanaokwamisha mradi Liganga na Mchuchuma kitanzani

Spread the love  NAIBU Spika wa Bunge, Mussa Zungu, watu wanaokwamisha utekelezaji...

Habari MchanganyikoTangulizi

Hii hapa kauli ya Sheikh mpya mkoa wa Dar

Spread the loveSAA chache baada ya kuteuliwa kukaimu nafasi ya aliyekuwa Sheikh...

Habari MchanganyikoTangulizi

Breaking news! Mufti amng’oa Sheikh mkoa Dar

Spread the loveBARAZA la Ulamaa la Bakwata katika kikao kilichofanyika tarehe 1...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali yatoa tamko bungeni sakatala la viboko shuleni

Spread the love  SERIKALI imewaagiza maafisa elimu wa mikoa na wilaya kuratibu...

error: Content is protected !!