May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Messi aoneshwa kadi nyekundu ya kwanza

Spread the love

MSHAMBULIAJI na Nahodha wa timu ya FC Barcelona, Lionel Messi ameoneshwa kadi nyekundu kwa mara ya kwanza tangu alipoanza kuitumikia klabu hiyo kwenye mchezo wa fainali wa kombe la Super Cup dhidi ya Atletic Bilbao. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea)

Kwenye mchezo huo ambao Barcelona walipoteza kwa mabao 3-2, Messi alioneshwa kadi hiyo dakika 121, wakati wa muda wa nyongeza mara baada ya kumpiga kichwani mchezaji wa Atletic Bilbao, Asier Villalible.

Mara baada ya kuoneshewa kadi hiyo na kwenda nje iliwachukua dakika tatu Atletic Bilbao kupachika bao la tatu lililodumu mpaka mwisho wa mchezo na kufanya Bilbao kutwaa ubingwa wa Super Cup.

Hii itakuwa kadi ya pili nyekundu kwa mchezaji huyo, huku moja aliipata akiwa na timu ya Taifa ya Argentina.

Toka alipojiunga na klabu hiyo 2004, Messi amecheza jumla ya mechi 753 za mashindano mbalimbali kwa muda wa miaka 17 bila ya kuoneshwa kadi nyekundu.

error: Content is protected !!