Monday , 30 January 2023
Home Kitengo Michezo Messi afungua akauti ya mabao PSG
Michezo

Messi afungua akauti ya mabao PSG

Spread the love

 

Mshambuliaji wa mpya wa klabu ya PSG Raia wa Argentina Lionel Messi amefungua rasmi akauti ya mabao katika klabu yake hiyo, mara baada ya jana kupachika bao moja kwenye ushindi waliopata wa mabao 2-0, kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya dhidi ya Manchester City. Damas Ndelema TUDARCo….. (endelea)

Mchezo huo wa kundi A Ulipigwa jana kwenye dimba la Parc Des Princes na wenyeji Psg kufanikiwa kuondoka na pointi tatu.

Mchezaji huyo hakua na mwanzo mzuri katika klabu yake hiyo mpya kama wengi walivyotarajia baada ya kucheza michezo kadhaa bila kushinda tofauti na mpinzani wake mkubwa Cristiano Ronaldo ambaye alikua na mwanzo mzuri katika klabu yake mpya ya Manchester United.

Messi ilimlazimu kusubiri mpaka siku ya jana na kufunga goli hilo katika mchezo wa Ligi ya mabigwa barani Ulaya  dhidi ya Manchester City ambapo goli la kwanza la uongozi likifugwa na mchezaji  Idrissa Gueye ‘’Gana’’

Pia michuano hiyo iliendelea kwa kupigwa mechi mbalimbali baada ya kushuhudia Liver pool wakiubuka na ushindi mnono ugenii wa  mabao 5-1 dhidi ya FC porto ya nchini ureno , huku mabigwa mara kumi na tatu wa michuano hii ya klabu bigwa barani Ulaya timu ya Real Madrid wakikubaki kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Sheriff Fc ya nchini Moldovia na kufanya waongoze kundi wakiwa na jumla ya pointi sita , pia Ac milan walichoshana nguvu na Atletico Madridi kwa kutoka sare ya bao1-1, Dortmund 1 Vs 0 Sporting cp , Leipzing1 Vs Club Brugge , shakhtar Donestk 0 Vs 0  Inter Milan

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

GGML: Uwanja mpya wa Geita Gold FC kukamilika Mei, 2023

Spread the loveUWANJA wa Magogo unaojengwa na Halmashauri ya Mji wa Geita...

Michezo

Wanafunzi chuo Mwalimu Nyerere wapongezwa kwa ushindi

Spread the love  UONGOZI wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA)...

Michezo

Arsenal waipopoa Manchester United

Spread the loveKLABU ya Arsenal inayoshiriki Ligi Kuu England imewatandika Mashetani Wekundu...

Michezo

Mchezaji Singida apoteza maisha mazoezini

Spread the love  MCHEZAJI na kapteni wa timu ya vijana ya Singida...

error: Content is protected !!