January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mengi: Wawekezaji wa ndani waaminiwe

Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Dk. Reginald Mengi (wa pili Kulia), akimkabidhi zawadi ya Sh. 5 milioni mshindi wa ku – tweet Antony Mhanda.

Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Dk. Reginald Mengi (wa pili Kulia), akimkabidhi zawadi ya Sh. 5 milioni mshindi wa ku – tweet Antony Mhanda

Spread the love

MWENYEKITI Mtendaji wa IPP, Dk. Reginald Mengi, amewataka viongozi wa Serikali kuwaamini wawekezaji wa ndani badala ya kuwaona wageni ndio wenye uwezo katika masuala ya uwekezaji. Anaandika Pendo Omary … (endelea).

Mengi ni mwasisi wa shindano la mtandao wakijamii wa Twitter kuhusu njia mbalimbali za kupambana na umasikini kupitia akaunti yake. Ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam wakati akitoa zawadi kwa washindi 10 wa shindano hilo kwa Aprili mwaka huu.

“Nchi yetu imekubwa na saratani yenye sura tata. Rushwa, ubinafsi na uongo. Sura hizi tatu za hii saratani inayotafuna nchi yetu ni lazima vijana muwe mstari wa mbele kusema bila kumung’unya maneno,” amesema Mengi.

Ameeleza kuwa “lazima nchi yetu itumie kwanza uwezo wa ndani na pale ambapo tumeshidwa kupata mtu mwenye uwezo ndani ya nchi ndipo tutumie wawekezaji kutoka nje,”

Aidha, tofauti na mashindano yaliyotangulia ambapo mshindi mkuu huwa mmoja anayepewa zawadi ya Sh. 10 milioni, shindano la mwezi huu limeibua washindi wakuu wawili.

 Jopo la majaji lililoongozwa na Dk. Donath Olomi – Mwenyekiti wa kampuni ya Institute of Management and Entrepreneurship Development limelazimika kuwapa Sh. 5 milioni kila mmoja huku walioingia hatua ya 10 bora wakipata Sh. milioni moja kila mmoja.

Washindi hao wawili ni David Fabian Moyambwa ambaye wazo lake lililenga kuanzisha mfumo wa ulinzi shirikishi kupitia simu za mikononi ambao utaiunganisha jamii katika njia moja itakayoashiria uhalifu ukitokea.

Mshindi mwingine ni Antony Mhanda ambaye wazo lake linahusu kujenga maabara ndogo ya kuchakata na kupima ubora wa asali ya wafugaji na kusindika mkoani Katavi.

Washindi wengine walioingia kumi bora ni: Dafroza Kataraihya, Phelemon Naman, Salehe Senkondo, David Dee, Freddy Freddy, Deodatus Mramba, Mbonea Mpembeni na Yusuph Maglah.

error: Content is protected !!