Saturday , 13 April 2024
Home Kitengo Michezo Meneja wa Simba atupwa ‘jela’ ya soka
Michezo

Meneja wa Simba atupwa ‘jela’ ya soka

Meneja wa Simba, Robert Richard
Spread the love

KAMATI ya Maadili ya Shirikisho la Mpira Miguu Tanzania (TFF) kupitia mwenyekiti wake Hamidu Mbwezeleni imemfungia Meneja wa Simba, Robert Richard kutojihusisha na soka kwa kipindi cha mwaka mmoja pamoja na faini ya shilingi 4, baada ya kukutwa na makosa mawili ya kimaadili. Anaripoti Kelvin Mwaipungu. … (endelea).

Kosa la kwanza alilokutwa nalo meneja huyo ni kuhujumu timu ya Taifa kwa kutotii wito wa TFF na kosa la pili kuchelewesha kuwapa taarifa kwa wakati wachezaji wa Simba kujiunga na timu ya Taifa ili kujiandaa na mchezo wa kufuzu kombe la mataifa Afrika dhidi ya Uganda uliochezwa mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye Uwanja wa Nelson Mandela uliopo Nambole.

Hapo awali ikumbukwe Kocha mkuu wa Taifa Stars, Emmanuel Amunike aliwaondoa kwenye kikosi wachezaji sita wa kikosi cha Simba kwa kosa la kuchelewa kuripoti kambini katika muda muafaka.

Wachezaji hao ni Jonas Mkude, Hassan Dilunga, Shomari Kapombe, John Bocco, Shiza Kichuya na Erasto Nyoni.

Meneja huyo kuanzia sasa hatoonekana kwenye benchi la klabu ya Simba kwa michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara na hata ile ya klabu bingwa barani Afrika kutokana na kuwepo kifunguni kwa mwaka mzima.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Usiku wa Ulaya kinawak tena leo

Spread the love  LIGI ya mabingwa barani ulaya itaendelea tena leo ambapo...

Michezo

Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya ni Usiku wa Kisasi

Spread the love  LEO utarejea ule usiku pendwa kabisa kwa mashabiki wa...

BurudikaMichezo

Kizz Daniel aunguruma na EP mpya ‘Thankz alot’

Spread the loveMKALI wa muziki nchini Nigeria, Kizz Daniel ametoa EP yake...

MichezoTangulizi

Samia aipa tano Yanga

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan ameipongeza Klabu ya Yanga licha ya...

error: Content is protected !!