Friday , 9 June 2023
Habari za SiasaTangulizi

Membe: Tumekimbiwa

Benard Membe, Mgombea Urais kwa tiketi ya ACT-Wazalendo
Spread the love

BERNARD Membe, mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha ACT-Wazalendo amesema, mazingira magumu ya siasa kwa sasa, yamesababisha marafiki na wafanyabiashara kushindwa kuwasaidia. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Na kwamba, kusuasua kwa kampeni hasa vyama vya upinzani nchini, kunatokana na ukweli kwamba, wagombea wengi wana ukata kwani hawana msaada tofauti na chaguzi zilizopita.

Membe amabye alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje katika Serikali ya Awamu ya Nne, ametoa kauli hiyo leo tarehe 15 Septemba 2020, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam muda mfupi baada ya kurejea nchini akitokea Dubai.

“Mnapokuwa katika mbio za urais, unatakiwa ukae ujipange kifedha na uwe na timu za kampemi,  vyama vyote vyenye wagombea, wana ukata wa fedha sababu vyanzo vyetu vinavyokubalika kisheria, wafanyabiasha wanaotoa msaada wote wamekimbia, hatuna fedha,” amesema Membe.

Amesema, kikwazo kingine ni mazingira ya sasa ambayo hayaruhusu kutoa wala kuingiza fedha ndani ya nchi, jambo ambalo linasababisha ugumu wa kampeni.

“Sababu nyingine, tunazuiliwa muingiza fedha, ukitaka kuingiza ama kutoa fedha, unakataliwa. Nikiwa rais, nitaboresha mfumo wa fedha kuiondoa changamoto hiyo,” ameahidi Membe.

Akielezea sababu za kushindwa kuendelea na kampeni za urais kwa mujibu wa ratiba yake, amesema waliamua kusitisha kwa kuwa baadhi ya wagombea wa ubunge na udiwani kwenye chama chake waliwekewa pingamizi.

“Kilichotokea, baada ya kuteuliwa mgombea wa urais, sisi  wabunge wetu zaidi ya 40 waliwekewa pingamizi.

Sasa akili inakutaka utafute changamoto ya tatizo kwanza. Huwezi kukurupuka peke yako, unawaacha wabunge na madiwani wamewekea pingamizi,” amesema Membe.

Akizungumzia safari yake ya Dubai Membe amesema, alikwenda kwa kuwa, ni ratiba yake ya kawaida kwa maana ndani ya mwaka mmoja anapaswa kwenda mara nne kutokana na shughuli zake binafsi.

“Kuna malalamiko kwanini ameenda Dubai kipindi hiki, huwa naenda Dubai mara nne kwa mwaka, kuna kampuni mimi ni mwanachama, sasa sikwenda mara mbili sasa nimeenda, lakini pia nimekwenda kucheki afya yangu,” amesema Membe.

2 Comments

  • Ugumu wa kampeni unasababishwa na ugumu wa kuingiza fedha kutoka nje??
    Kwani alitaka fedha za kampeni zitoke nchi gani? Anategemea wafadhili kutoka nje?? DU

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaTangulizi

Ngoma bado mbichi mkataba wa Bandari

Spread the love  SAKATA la mkataba wa uendeshaji, uendelezaji na uboreshaji wa...

BiasharaTangulizi

Mkurugenzi TPA: Mkataba unaweza kuvunjwa

Spread the loveMKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA),...

BiasharaTangulizi

Mkurugenzi TPA: Mikataba ya utekelezaji bado haijasainiwa

Spread the loveMKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA),...

Habari za Siasa

Lussu: Mkataba wa DP bandarini si wa miaka 100

Spread the loveMAKAMU Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, amesema hakuna ukweli wowote...

error: Content is protected !!