Saturday , 20 April 2024
Habari za SiasaTangulizi

Membe tishio CCM

Bernard Membe
Spread the love

CHAMA Chama Mapinduzi (CCM), kina hofu na Bernard Membe, Waziri wa Mambo ya Nje wa zamani. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Taarifa zilifikia mtandao huu zinaeleza, hatua ya Membe kutekenya nafasi ya urais kwenye uchaguzi mkuu ujao kupitia chama hicho, kunaweza kukipasua chama hicho.

“Nitakueleza kwa ufupi tu, unadhani watu wote ndani ya chama wanaridhika na mwenendo wa sasa? Jibu ni hapana. Sio jambo lingine isipokuwa wamekatwa midomo. Hakuna kitu kibaya kama kuwafunga watu midomo.

“Anapotokea mtu akasema hapana, this is not fair (hii sio haki), hata wale walioshindwa kujitetea bila shaka, wanakuwa nyuma ya yule jasiri hata kama hawana maslahi naye sana,” ameeleza ofisa mmoja wa CCM anayehudumu kwenye ofisi ndogo (Lumumba), jijini Dar es Salaam.

Amesema, suala la mwenyekiti wa sasa wa chama hicho (Dk. John Magufuli), kugombea urais si swala la kikatiba “na ndio maana Membe anaweza kupeleka jina na inakubalika.”

Jana tarehe 27 Novemba 2019, Dk. Bashiru Ally ambaye ni katibu mkuu wa chama hicho, alimtaka Membe kufuata taratibu za chama katika hatua zake kufikia dhamira yake, na kwamba hayupo juu ya katiba ya chama hicho.

Amesema, “Membe ni mwanachama mwenye haki ya kikatiba lakini ana wajibu.  Kwa hiyo kama anataka kuwa mwanachama wa CCM kama walivyo wengine, lakini wametupa ushindi tunaojivunia afutae utaratibu. Asipofuata utaratibu, atalazimishwa kufuata utaratibu,” ameeleza Dk. Bashiru.

Kauli hiyo inatokana na dhamira ya wazi aliyoionesha Membe siku za nyuma, kutaka kugombea urais kwenye uchaguzi mkuu 2020 kupitia chama hicho.

Membe amewahi kutuhumiwa kuendesha mikakati ya kutaka kumkwamisha Rais John Magufuli kuelekea uchaguzi mkuu mwakani.

Kutokana na kukomaa kwa tuhuma hizo, Dk. Bashiri alimtaka Membe kufika ofisini kwake kujibu tuhuma hizo. Hata hivyo, Membe hakuhojiwa.

“Tuna rekodi mbaya katika chama, mgombea urais akinuna tunapata tabu sana, na hatutaki kuendeleza mnuno wa wale wanaotafuta vyeo wakivikosa wanatuvuruga.

“Nalisema kwa vyeo vyote wagombea urais, ubunge, udiwani, hatutaki makundi tena katika chama chetu, tumeumizwa vya kutosha na makundi, uongo, fitina, ubinafsi, ubaguzi na matumizi mabaya ya fedha katika siasa, tulifikia mahala wagombea wa CCM wanaomba kura makanisani,” alinukuliwa Dk. Bashiru wakati akitoa ‘mwaliko’ kwa Membe.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Dk. Mwakyembe : Zanzibar waliongoza kutaka Serikali 2 za muungano

Spread the love  MWANASIASA mkongwe nchini, Dk. Harrison Mwakyembe, amesema mjadala wa...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataja mikakati ya kufikia trilioni 2 biashara Uturuki, Tz

Spread the loveWakati Tanzania na Uturuki zikidhamiria kuongeza kiwango cha biashara hadi...

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

error: Content is protected !!