October 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Membe: Ni kikao kigumu

Bernard Membe, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,

Spread the love

BERNARD Membe, waziri wa zamani wa Mambo ya Nje, leo tarehe 6 Februari 2020, anakwenda kuhojiwa na Kamati ya Kamati ya Maadili na Usalama ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma…(endelea).

Katika mahojiano na Azam jana tarehe 5 Februari 2020, Membe amesema kikao cha leo kitakuwa kigumu, na kwamba itategemea na mazingira atakayoyakuta.

Kuhusu kukubaliana na uamuzi utaotolewa leo, Membe alimwambia mwandishi wa kituo hicho kwamba ‘itategemea.’

Kwenye kikao, pamoja na wajumbe wengine, kitaongozwa na Philip Mangula, Makamu Mwenyekiti wa CCM. Membe aliianza safari ya kwendo Dodoma jana, kwa ajili ya kuhudhuria mbele ya kamati hiyo.

“Kamati itasikiliza hoja na watatoa mapendekezo,” amesema Membe na kuongeza “nadhani uamuzi utatoka mwishoni mwa mwa Februari au Machi.”

Membe mwenye kujiamini, amesema alikuwa na hamu na wito huo baada ya Halmashauri Kuu ya chama hicho tarehe 13 Desemba 2019, kuagiza Membe, Abdulrahman Kinana na Yusuf Makamba kufika mbele ya kamati hiyo kujieleza kutokana na tuhuma za kukosa maadili.

Hata hivyo, zilipita wiki kadhaa bila kamati hiyo kuwaandikia barua ya wito, juzi Membe alithibitisha kupokea barua inayomtaka kufika mbele ya kamati hiyo.

“hatimaye, jana (juzi) jioni nimepokea barua ya kuitwa kwenye kikao cha kamati ndogo ya udhibiti na nidhamu jijini Dodoma.”

Maneno yake ya awali aliyoyatoa Membe baada ya taarifa za kutakiwa mbele ya kamati hiyo kabla ya barua, ndio yale yale aliyoyatoa hata baada ya kupata barua hiyo.

Alisema ‘nina hamu na kamati hiyo’ akionesha kutokuwa na wasiwasi wowote. Tarehe 14 Desemba 2026, siku moja baada ya Halmashauri Kuu ya chama hicho kuielekeza kamati ya maadili kumwita Membe na wenzake, aliandika;

“Kutokana na wingi wa meseji, nashindwa kumjibu kila mtu aliyeniandikia ujumbe kuhusu tangazo la kuitwa kwangu. Niseme tu kwamba, nasubiri kwa hamu barua ya wito.”

error: Content is protected !!