Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Tangulizi Kauli ya Nape yamuibua Membe
Tangulizi

Kauli ya Nape yamuibua Membe

Spread the love

WIKI moja baada ya mwanasiasa nguli nchini, Benard Membe kurejea rasmi ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) tangu alipofukuzwa mwaka 2020, hatimaye ameeleza kuhusu kauli tata iliyotolewa siku ya kukaribishwa kwake. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Mei 29, mwaka huu Waziri huyo wa Mambo ya Nje ya Nchi wa zamani alikaribishwa tena ndani ya CCM baada ya miaka miwili aliyoishi nje ya chama hicho, akihamia ACT-Wazalendo na baadaye kutangaza kuachana nacho na kubaki kuwa mshauri wa kisiasa.

Wakati wa ukaribisho wake, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye alitoa kauli kuwa, “Bahari imetulia, Mwenyezi Mungu ameamua ugomvi, basi baki nyumbani tusonge mbele pamoja”.

Kauli hiyo iliibua mitazamo tofauti kutoka kwa baadhi ya wananchi wakitamani kujua ugomvi uliomalizwa na Mungu ni upi, huku tafsiri za baadhi yao zikijielekeza kwenye ugomvi wa kufukuzwa kwake CCM?

Ingawa kufukuzwa kwa Membe ndani ya CCM kulitokana na kile Kamati Kuu ya chama hicho ilichokieleza kuwa ni mwenendo wa kujirudia makosa na licha ya kupewa adhabu nyingine lakini hakujirekebisha.

Nape Nnauye, Mbunge wa Mtama

“Uamuzi huu umekuja baada ya kuwa taarifa zake (Membe) ndani ya chama zinaonyesha mwenendo wake kutoka mwaka 2014 ambako katika chama amewahi kupata adhabu nyingine ambazo zingeweza kumsaidia kujirekebisha lakini imeonekana sivyo,” alisema aliyekuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole, Februari 28, 2020.

Akifafanua kuhusu kauli ya Mungu ameumaliza ugomvi, Membe alisema ikilenga kuwaeleza wananchi wa Tarafa ya Rondo aliokuwa na ugomvi nao kwamba sasa umemalizika.

Alisema kufukuzwa kwake ndani ya CCM kuliibua hasira miongoni mwa wananchi, hatua ambayo ilisababisha katika moja ya mkutano wa Nape kuhudhuriwa na watu 12 pekee.

“Kwa sababu watu walikuwa na hasira na wakabishana pale …. Mimi mwenyewe sikuwepo. Nilipata tabu sana kama mbobevu, kama mataafu, kama mtu ambaye nilimshabikia Nape Nnauye.

“Sasa tumekwenda na hiyo misuguano hadi niliporejea CCM na Nape alikuwa miongoni mwa viongozi ndani ya chama waliokuwa wanakuja kila mwezi kuniomba nirejee CCM. Nikarejea CCM,” alisema.

Baada ya kurejea CCM, alisema alizungumza na wananchi na kuwaeleza kuwa “yaliyopita si ndwele tugange yajayo” na kusisitiza kuwa mtafaruku ya yao na Nape umalizike.

“Nilimtaka Nape alieleze hilo, sasa Nape ni msomi na mwanasiasa, akaliweka kwa lugha aliyoliweka. Kwa hiyo wananchi wa Rondo kauli ya Nape ni ya kueleza kwamba mgogoro wa wananchi wa Rondo na mbunge ambao walikuwa nao sasa umekwisha hiyo ndiyo tafsiri tuliyoipata,” alisema.

Kinyume na tafsiri hiyo, Membe alisema magazeti yalikuja na yao ambayo hata yeye hakuwa kiuzungumzia.

Miaka miwili akiwa nje ya CCM, Membe aligombea urais wa Tanzania kupitia chama cha ACT-Wazalendo alichojiunga nacho Julai 15, 2020 miezi kadhaa baada ya kufukuzwa CCM.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

Habari za SiasaTangulizi

CAG aibua madudu halmashauri 10, TANESCO na MSD

Spread the loveRIPOTI ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali...

error: Content is protected !!