October 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Membe ataja mambo matatu ya JPM yaliyomkuna

Spread the love

BERNALD Kamillius Membe, waziri wa zamani wa mambo ya nje katika serikali ya awamu ya nne, amefurahishwa na mambo matatu yaliyofanywa na Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Amesema, katika uongozi wa Rais Magufuli kuanzia alipoingia madarakani tarehe 5 Novemba 2015 mpaka sasa, anamsifu kwa mambo matatu makubwa.

Akizungumza na Sammy Awami, Mwandishi wa BBC nyumbani kwake Lindi, Membe ametaja mambo hayo ni kupambana na rushwa, ujenzi wa miundombinu na kuwapa fursa vijana.

“Mambo matatu mimi yamenifurahisha, moja: maendeleo ya miundombinu, rais (huko nyuma) amekuwa waziri wa miundombinu na ameendeleza hiyo,” amesema.

Membe ambaye awali alikuwa Mbunge wa Mtama amesema, barabara nyingi nchini zimejengwa katika kipindi cha miaka mitano ya uongozi wa Rais Magufuli ikiwa ni pamoja na ujenzi wa reli ya kati na barabara za juu (flying overs), “haya ni mambo mema,” amesema.

Bernard Membe (kulia) akisalimiana na Rais John Magufuli walipokutana katika mkutano Mkuu wa CCM 2015

Akitaja jambo la pili, Membe amesema, kwenye utawala wake Rais Magufuli amewapa fursa vijana na kwamba vijana ni wengi kwenye utawala wake kuliko awamu zilizopita.

“Rais amewakumbatia vijana katika uongozi huu, nadhani kwa wingi zaidi kuliko sisi ingawa anawatumbuatumbua,” amesema Membe.

Akitaja jambo la tatu, Mwanadiplomasia huyo, amesema Rais Magufuli amepambana na rushwa ingawa kuna maeneo bado.

“Tunapozungumzia suala la rusha, yapo maeneo ameyaacha nafikiri labda anasubiri second term (awamu ya pili), lakini yamo maeneo ameyashughulikia vizuri,” amesema

“So (hivyo) suala la miundombinu, rushwa na ukumbatiaji wa vijana ni vitu ambavyo mimi pia ningevifanya. Kwa upande huo amefanya vizuri,” amesema Membe ambaye alikuwa miongoni mwa wana CCM 42 waliochuana kumrithi Rais mstaafu Jakaya Kikwete.

Ubungo interchange

Hata hivyo, Membe hakupenya na Rais Magufuli akaibuka mshindi ndani ya CCM na Watanzania wakamchagua kuwaongoza.

Akizungumzia uhuru wa vyombo vya usalama amesema, vyombo vivyo vinategemea kwa kiasi kikubwa rais aliyepo madarakani.

“Uhuru ni kitu cha msingi sana cha uongozi bora, Uhuru wa Mahakama, Uhuru wa Bunge yaani liingiliwe na liwe linafanya kazi zake kwa mujibu wa sheria bila kuingiliwa, mipaka hiyo ipo rasmi kwenye Katiba na haitakiwi kuingiliwa.”

“Behavior (tabia) ya vyombo vya usalama inategemea na uongozi uliopo. Kwa sababu, amiri jeshi mkuu anayo haki ya kutoa amri ya kuelekeza na kutaka vyombo vyake vifanye nini. kwa hiyo, inategemea na nani yupo kwenye madaraka,” amesema.

error: Content is protected !!