September 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Membe arejesha fomu za urais, atumia saa 48 kuzijaza

Spread the love

BERNARD Kamilus Membe, waziri wa zamani wa mambo ya nje, amerejesha fomu za kuomba kuteuliwa na chama cha upinzani cha ACT-Wazalendo kuwania urais wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Membe amerejesha fomu hizo Ofisi ya ACT Wazalendo Magomeni, Dar es Salaam leo Jumapili tarehe 19 Julai 2020 na kupokelewa na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho-Bara, Joran Badhange.

Fomu hizo alizichukua ofisini hapo siku mbili zilizopita (sawa na saa 48) tarehe 17 Julai 2020 ambapo alikabidhiwa na Ado Shaibu, Katibu Mkuu wa ACT-Wazalendo.

Tofauti na alivyosema wakati akichukua fomu hizo kuwa wakati akirejesha fomu hizo atazungumza maneno mawili matatu, hali imekuwa tofauti, kwani hakuzungumza lolote.

Bernard Membe, waziri wa zamani wa mambo ya nje, akikabidhi fomu ya kuomba kuteuliwa na chama cha ACT-Wazalendo ili kugombea urais wa Tanzania katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 2020 Naibu Katibu Mkuu Bara Joran Bashange

Membe amejiunga na chama hicho tarehe 7 Julai 2020 akitokea chama tawala Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambako alifukuzwa uanachama tangu tarehe 28 Februari 2020 kwa madai ya kukiuka miongozo na taratibu za chama hicho tangu mwaka 2014.

error: Content is protected !!