October 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Membe amfagilia Rais Samia, ampa ujumbe Majaliwa

Spread the love

 

ALIYEWAHI kuwa waziri wa mambo ya nje wa Tanzania, Bernard Membe amesema Rais Samia Suluhu Hassan ni kiongozi jasiri na mahiri, anatosha kuiongoza Tanzania na anamuunga mkono kwa kazi kubwa anayoifanya. Anaripoti Mwandishi Wetu, Lindi … (endelea).

Membe ameyasema hayo leo Jumanne tarehe 4 Oktba 2020 alipozungumza mbele ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, ambaye yuko katika ziara ya kikazi ya kukagua miradi ya maendeleo Mkoani Lindi.

Membe amemuomba Waziri Mkuu afikishe salamu zake pamoja na za wananchi wa kijiji cha Rondo kwa Rais Samia kwamba wanamuunga mkono katika jitihada kubwa za kuwaletea wananchi maendeleo.

Rais Samia Suluhu Hassan

“Mheshimiwa Waziri Mkuu naomba ufikishe salamu zetu sisi Wana-Rondo kwa Mheshimiwa Rais Samia mwambie tunampenda, anatosha na tutamsaidia,” anesema Membe ambaye alikuwa mgombea urais wa Tanzania, katika uchaguzi mkuu 2015 kupitia ACT-Wazalendo.

Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Rondo, Majaliwa amewasihi wananchi hao wawapeleke watoto shule, kuanzia ngazi ya elimu ya awali na shule za Sekondari kwani Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imeweka msisitizo katika kuhakikisha kila Mtanzania anapata elimu bora.

Aidha, Waziri Mkuu ametoa onyo kali kwa vijana na watu ambao wamekuwa wakiwarubuni wanafunzi wa kike kuacha masomo na wengine kuwapa mimba waache ili watoto hao waweze kutimiza ndoto zao.

error: Content is protected !!