July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Membe ahofu ugaidi Mashariki ya kati

Bernard Membe, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,

Spread the love

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, amekiri kuwa kushamili kwa vitendo vya kigaidi katika nchi za Mashariki na Kati, kunaleta tishioa la amani kwa nchi hizo. Anaandika Dany Tibason … (endelea).

Akiwasilisha hotuba ya bajeti ya makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2015/16, Membe amelieleza Bunge kuwa, vikundi hivyo vimesababisha amani na usalama katika maeneo ya mashariki na kati kuzorota hasa baada ya wimbi la baadhi ya makundi kuanzisha vurugu na vita kwa madai ya demokrasi na utawala wa sheria katika nchi za Kiarabu.

Hata hivyo, amesema hali ya amani na usalama barani Afrika kwa kipindi cha mwaka 2014/15 imezidi kuimarika.

Licha ya kuimarika kwa amani na usalama lakini bado juhudi zinaendelea ili kutafuta suluhu ya migogoro ya kisiasa ambayo inaendelea kwenye nchi za Sudan Kusini, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).   

Kuhusu mpaka baina ya Tanzania na Malawi kwenye Ziwa Nyasa, Membe amesema bado suala hilo lipo katika hali ya masuluhisho na halijapatiwa ufumbuzi.

Amesema kuwa, katika mkutano wa mwisho uliofanyika Machi mwaka jana, pande zote mbili pamoja na msuluhishi zilikubaliana kuwa mchakato huo usogezwe mbele mpaka baada ya uchaguzi mkuu wa Malawi uliofanyika Juni mwaka jana.

Kuhusu utekelezaji wa majukumu ya wizara kwa mwaka wa fedha 2014/15, Membe amesema kuwa kwa kushirikiana na idara na taasisi nyingine za serikali na sekta binafsi, wameendelea kutekeleza majukumu yake ipasavyo.

Akizungumzia mabadiliko ya tabianchi, amesema kuwa hali hiyo ni tishio kubwa kwa ukuaji na ustawi wa dunia nzima. Kwamba, hali hiyo inathibitishwa na matokeo ya vimbunga, ukame, mafuriko, magonjwa na kupotea kwa baadhi ya wanyama na mimea.

Kwa mujibu wa Membe, kutokana na hali hiyo, ushiriki wa Tanzania kwenye mikutano ya mabadiliko umeimarishwa.

error: Content is protected !!