July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Meli kupitisha mafuta TPA Tanga

Bandari ya Tanga

Spread the love

MAMLAKA ya Udhibiti wa Nishati, Maji na Mafuta Tanzania (EWURA), imeutaarifu umma kuwa, Bandari ya Tanga inatarajiwa kuanza kutumika kupitishia meli za mafuta tena mwazoni mwa Julai mwaka huu. Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).

Aidha, lengo la huduma hiyo kuanza mkoani humo ni kuondoa msongamano wa  meli za mafuta ziingiazo katika Bandari ya Dar es Salaam.

Taarifa hiyo imetolewa leo katika kikao kilishoshirikisha wadau  mbalimbali nchini ambapo mamlaka hiyo  ilikusanya maoni juu ya mradi wa bandari ya Tanga pamoja na kutatua changamoto ya uingiaji wa mafuta nchini.

Hayo yalisemwa Jijini Dar es Salaam na  Mkurugenzi Mkuu EWURA, Felix Ngamlagosi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambamo  amesema lengo la kuanza tena kuitumia bandari ya Tanga ni kuweza kuepusha gharama za usafirishaji.

Amesema, kitu kingine kilichowapelekea kushusha mafuta bandari ya Tanga ni kuweza kurahisisha gharama za usafirishaji wakati wa kusambaza mafuta mikoa mingine.

Ngamlagosi amesema, pia wanampango wa kuinua uchumi wa Tanga kwa kuboresha miundo mbinu mbalimbali zikiwemo barabara za kusafirishia mafuta hayo.

“Tunategemea kuwa na bei sawa za mafuta kwa upande wa Dar na Tanga, ili kuwasaidia walaji kununua kwa bei nafuu. pesa itakayopungua katika usafirishaji itatumika kuboresha miundo mbinu ya barabara.” amesema Ngamlagosi.

error: Content is protected !!