Saturday , 20 April 2024
Home Habari Mchanganyiko MEI MOSI – Waajiri walia mrundikano wa kodi
Habari Mchanganyiko

MEI MOSI – Waajiri walia mrundikano wa kodi

Spread the love

CHAMA cha Waajiri Tanzania (ATE) kimesema mrundikano wa kodi zinazotozwa na taasisi mbalimbali za Serikali, umesababisha waajiri kupunguza wafanyakazi. Anaripoti Mwandishi Wetu… (endelea).

Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 1 Mei, 2022 Mwenyekiti ATE, Jayne Nyimbo katika maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi Duniani yaliyofanyika jijini Dodoma.

Pia katika maadhimishi hayo ambayo mgeni rasmi ni Rais Samia Suluhu Hassan, Nyimbo ametoa wito kwa waajiri kutopa fursa kwa wahitimu kujifunza kwa vitendo ili kupunguza changamoto ya uzoefu kazini.

“Waajiri tunakabiliwa na changamoto nyingi hasusani katika masuala ya mrundikano wa kodi tunazotozwa na mamlaka mbalimbali hali inayoongeza gharama za kufanya biashara na ugumu wa mazingira ya kufanya biashara.

“Baadhi ya waajiri hujikuta wakilazimika kupunguza wafanyakazi hasa kwenye sekta zilizoathiriwa na janga la Ukimwi na Uviko – 19, mathalani sekta ya utalii na ukarimu,” amesema Mwenyekiti huyo.

Aidha, Nyimo ametoa wito kwa waajiri na wafanyakazi kuendelea kushirikiana na serikali kujenga uchumi, kufanya kazi kwa bidii na kulipa kodi stahiki.

“ATE ambaye ni mwakilishi wa waajiri kutoka sekta binafsi tunaendelea kuwa sauti ya waajiri nchini na kufanya ushirikiano wa Serikali na vyama vya wafanyakazi ni ombi letu kwa wadau wa utatu kuendelea kushirikiana na kufanya kazi kwa pamoja ili kutatua changamoto katika sekta hii maana umoja ni nguvu,” amesema na kuongeza.

“Ombi letu kwako pia Mheshimiwa Rais Samia Suluhu kutupatia kiwanja kimoja hapa Dodoma ili ATE tuondokane na gharama za kupanga hapa Dodoma,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

Habari Mchanganyiko

Tanzania yachaguliwa Makamu wa Rais Tume ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Spread the love  TANZANIA kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)...

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

error: Content is protected !!