July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

MEDO kuwakomboa wasichana Morogoro

Msichana akinyonyesha mtoto baada ya kujifungua

Spread the love

TAASISI ya Maendeleo ya Elimu Morogoro (MEDO), inatarajia kujenga  kituo kikubwa cha  kuwasaidia watoto wa kike waishio katika mazingira magumu kwa kuwapatia elimu. Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).

Kituo hicho kitagharimu Sh. 230 million na kwamba kitajegwa mkoani Morogoro.

Akizungumza na waandishi leo Jijini Dar es Salaam, Meneja Mradi wa MEDO, Betha Gama amesema, lengo la ujenzi wa kituo hicho ni kuhakikisha watato wa kike wote waishio katika mazingira magumu wanapata elimu.

Gama amesema, lengo lingine ni kuweza kuisaidia serikali katika kutokomeza mimba za utotoni.

Amesema, sababu iliyowasukuma kujenga kituo hicho Morogoro ni kutokana na utafiti uliofanywa mkoani humo ambapo ulibaini kuwa, watoto wa kike wengi hawapati fursa ya kusoma kutokana na umaskini uliokithiri.

“Katika tafiti zetu, tulitembelea vitongoji vingi mkoani humo na tukaweza kukutana na familia nyingi zenye matatizo tofauti hususani kwa watoto wa kike. Ndipo MEDO iliamua kufuatilia histolia za watoto mbalimbali,” amesema Gama.

Amesema, MEDO huwapata watoto hao kwa kuwasiliana na viongozi mbalimbali wa kiserikali pamoja na waalimu wa shule za msingi  ili kupata watoto wenye mwelekeo na watakao weza kusaidika.

Mbali na hilo Gama amesema, MEDO kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imeendaa kampeni za kuelimisha na kuweza kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi huo.

“Tumeshirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo wasanii wa kike, ambao wapo tayari kuunga mkono ujenzi huo, ambapo watatumia vipaji vyao kuhamasisha jamii kujitolea mchango huo” amesema.

Aidha, kupitia kampeni hizo MEDO inatarajia kukusanya Sh. Millioni 400, zitakazoweza kuwasaidia watoto ndani ya kituo na kutoa misaada  kwa watoto wa aina zote wenye umaskini.

Kampeni hizo zitaambatana na kauli mbiu inayosema, “Nisaidie mimi mia tano inatosha kunipa elimu” .Kampeni zinatarajiwa kuanza mara baada ya mwezi wa ramadhani kuisha.

error: Content is protected !!