Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari MECIRA yafichua chanzo cha ukame, yataka Serikali iwachukulie hatua wahusika
HabariMazingira

MECIRA yafichua chanzo cha ukame, yataka Serikali iwachukulie hatua wahusika

Hali ya ukame katika moja ya maeneo ya Afrika kwa sasa
Spread the love

KITUO cha Wanahabari Watetezi wa Rasilimali na Taarifa (MECIRA), wameiomba Serikali iwachukulie hatua watu wanaofanya vitendo vya uharibifu wa mazingira, Kwa kuwa ndiyo chanzo cha matokeo ya ukame unaowaathiri wananchi. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Akizungumza na wanahabari leo Jumapili jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa MECIRA, Habib Mchange, amesema waharibifu wa mazingira wanaendelea kufanya shughuli za kibinadamu katika maeneo yasiyo stahiki, kutokana na baadhi ya watendaji wa Serikali kutofuata Sheria katika kuwadhibiti.

“Sababu hii nchi ni huru mimi mwanahanari sizuiwi kuwa mfugaji, kwa sababu hiyo tunakutana na changamoto watunga Sheria ambao wanajihusisha na shughuli nyingine zinazowahusu hivyo wanaweka Sheria Kwa kujilinda,” amesema Mchange.

Mchange amesema wajumbe wa MECIRA walifanya ziara katika mikoa kadhaa ili kubaini hali ya utunzaji wa mazingira ilivyo, ambapo waligundua vyanzo vya maji hususan vya Mto Ruaha, vimekauka kutokana na shughuli za kibinadamu.

“Tumeenda site Ruaha tumekuta kuna watu wameziba vyanzo vya maji, lakini wanatafuta ridhiki. Swali je wameeleweshwa vya kutosha? Nani mwenye mamlaka ya kuwaelimisha, ni wanahabari,” amesema Mchange.

Mbali na Mto Mkuu Ruaha ambao hauna maji kwa takribani siku 126, miongoni mwa mito mingine iliyoathirika ni Ruvu na Mtwara.

Amesema, ukame katika vyanzo vya maji ndiyo sababu ya changamoto ya mgawo wa maji na umeme inayowakabili wananchi, ambapo amewataka wanahabari kutumia kalamu zao kuuelimisha umma juu ya madhara ya kuharibu mazingira na vyanzo vya maji.

Mchange amesema MECIRA imeandaa kongamano litakalofanyika mkoani Iringa tarehe 19 Desemba 2022, ambapo wadau mbalimbali wa mazingira ikiwepo wanahabari, watapata nafasi ya kujadili Ili kujua chanzo cha matatizo ya uharibifu wa mazingira na suluhu zake.

Amesema, katika kongamano Hilo wadau watajadili Sheria zinazosimamia mazingira, Ili kama zinamapungufu waishauri Serikali namna ya kuziboresha ili kudhibiti uharibu wake na kuwachukulia hatua wanaoufanya.

Naye Mjumbe wa MECIRA, Manyerere Jackton, amesema Tanzania ni miongoni mwa mataifa yanayoathirika na tatizo la mabadiliko ya taifa ya nchi na ukame, hivyo amewataka wanahabari wasiwe walalamikaji bali watumie kalamu zao kuelimisha jamii ili iache tabia ya kuharibu mazingira na vyanzo vya maji.

“Kuna shughuli za kibinadamu zipo Ruaha, watu wamejenga ukuta kuzuia maji yasiende mtoni yaende shambani, mtu anajenga Kwa Sh. 500 milioni na wako wengi. Kuna mito mitano inapeleka maji Ruaha lakini hayafiki matokeo yake samaki na viboko wanakufa,” amesema Manyerere.

Manyerere amesema kuwa, katika ziara iliyofanywa na MECIRA kukagua uharibifu wa mazingira, ilibaini shughuli za uvuvi haramu katika baadhi ya maeneo, ambapo wahusika hutumia sumu na mashine za kunyonya maji kuyatoa nje ya mito ili wapate samaki Kwa urahisi.

“Kuna wafugaji wa hali ya juu ng’ombe wanakamatwa , wale ng’ombe sio wa malofa ni wa watu wazito. Tunaamini Dola wanatambya Hilo na pengine hatua zinaweza kuchukuliwa. Kuna watu wanaingiza mifugo mingi, siku Moja ng’ombr 800 waliingia wakaambiwa watoe faini ya Sh. 80 milioni wanalipa kesho wanarudia Tena,” amesema Manyerere.

Afisa Mahusiano wa MECIRA, Hamisi Mkotya, ameiomba Serikali ihakikishe watendaji wake wanafuata Sheria katika kudhibiti uharibifu wa mazingira.

“Sheria zipo, tunaiomba Serikali itekeleze Sheria sababu ukisoma Sheria inakwambia usijenge mita 60 kutoka chanzo Cha maji lakini watu wanajenga. Sheria zipo lakini Kuna ulegevu Kwa wanaosimamia, mtu anakwenda kuharibu mamlaka zipo wanaangalia,” amesema Mkotya.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

HabariSiasa

Dk. Rose Rwakatare atoa kadi 500 kila Wilaya Morogoro

Spread the loveMWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Morogoro, Dk...

ElimuHabari

CBE, WMA wasaini makubaliano wanafunzi kusoma wakifanyakazi

Spread the loveNAIBU Spika Musa Azzan Zungu amekipongeza Chuo cha Elimu ya...

HabariTangulizi

Dk. Slaa, Mwabukusi kuhojiwa na jeshi la Polisi Mbeya

Spread the loveJESHI la Polisi jijini Mbeya, linawashikilia kwa mahojiano Dk. Wilbroad...

HabariHabari Mchanganyiko

Kairuki Hospital Green IVF  yawanoa madaktari kuhusu upandikizaji mimba

Spread the love KITUO cha Upandikizaji Mimba cha Kairuki Hospital Green IVF...

error: Content is protected !!