May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mechi ya Uskochi na Ukrenia kufuzu kombe la dunia yaahirishwa

Kikosi cha timu ya Taifa ya Ukraine

Spread the love

 

MECHI ya nusu fainali katika michuano ya kufuzu fainali za kombe la dunia kati ya Uskochi na Ukrenia imeahirishwa. Inaripoti BBC … (endelea)

Mechi hiyo ilipangwa kuchezwa tarehe 24 Machi 2022 na sasa kuna uwezekano wa kuchezwa mwezi Juni mwaka huu.

Bodi ya uendeshaji FIFA imekubali ombi la lililotolewa wiki iliyopita na Shrikisho la mpira wa miguu la Ukrenia.

Mshindi wa nusu fainali hiyo inayotarajiwa kupigwa katika dimba la Hampden Park atacheza na ama Austria au Wales ili kufuzu fainali za kombe la dunia Novemba mwaka huu.

Ligi ya Ukrenia imesitishwa tangu Urusi iivamie nchi hiyo tarehe 24 Machi 2022.

Urusi imeondolewa katika michezo yote ya soka ya kimataifa na hawataweza kucheza mchezo wake wa mtoano na Poland.

error: Content is protected !!