May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mechi ya Simba na FC Platnum, yasababisha mateso kwa shabiki

Kibabu Nassoro

Spread the love

SIKU ya tarehe 6 Januari, 2021, ni siku ambayo haitasahaulika kwa familia ya Rehema Abdallah, baada ya kijana wao, Kibabu Nasoro (30) kupata ajali mbaya iliyopelekea kufanyiwa upasuaji wa kichwa na tumbo. Anaripoti Hamisi Mguta, Dar es Salaam … (endelea). 

Nasoro mkazi wa Kimara Jijini Dar es Salaam ni shabiki mkubwa wa timu ya Simba, alipata ajali siku hiyo akitokea kwenye mechi kati ya timu yake hiyo iliyocheza dhidi ya FC Platnum katika uwanja wa Mkapa, mechi iliyopachikwa jina la ‘War in Dar’.

Ama kweli, hakuna aijuae kesho, na laiti kama binadamu tungekuwa tunafahamu tatizo litatokea wakati fulani basi tungeweza kujiepuka mengi yasitokee.

Nasoro ana mtoto mmoja. Familia yake ilikuwa ikimtegemea kwa huduma na mahitaji mbalimbali kupitia kazi yake ya udereva wa magari makubwa, lakini utegemezi wake katika familia ulikoma baada ya ajali hiyo mbaya. Kijana huyu anapitia mateso nayoishi kwa kukosa msaada wa kumhudumia kimatibabu.

Hospitali wanadaiwa Sh. 800,000 lakini anahitajika kufanyiwa upasuaji mwingine wa kichwa, anahitaji msaada wa wadau.

Kumsaidia kijana huyu unaweza kuchangia ulicho nacho kupitia 0788 235 582 – Rehema Abdallah

Fuatilia simulizi hii kupitia MwanaHALISI TV

error: Content is protected !!