Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mdude ajitosa madai katiba mpya, atoa ahadi nzito
Habari za SiasaTangulizi

Mdude ajitosa madai katiba mpya, atoa ahadi nzito

Mdude Nyagali
Spread the love

 

KADA wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mdude Nyagali amekula kiapo cha kusaka katiba mpya, kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2025. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Akizungumza katika uzinduzi wa kongamano la katiba mpya lililofanyika jana Alhamisi, tarehe 1 Julai 2021 jijini Dar es Salaam, Mdude amesema, atahakikishia katiba mpya inapatikana.

“Niwaahidi kitu kimoja, hii katiba mpya haitavuka 2025 na niwaambie ni mwisho wa wakurugenzi kusimamia uchaguzi na kama vijana mnaogopa, nitasimama peke yangu kuitafuta katiba mpya. Kuna wakati ni lazima kutumia njia isiyo sahihi kuipata njia iliyosahihi,” amesema Mdude.

Mdude amesema, anajitosa katika mchakato wa kudai marekebisho ya katiba, ili aache alama kwa Taifa.

“Mimi kama kijana, nina jukumu la kuidai katiba mpya, nguvu niliyonayo ni mara mia na ninawaahidi kabla 2025 tutapata katiba mpya, nawaapia vijana mjiandae msirudi nyuma. Msikate tamaa mnapaswa kuacha alama kama watangulizi,” amesema Mdude.

Mdude ametoa ahadi hiyo siku tatu baada ya Mdude kuachwa huru na Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya, tarehe 28 Juni 2021, kutomtia hatiani katika kesi iliyokuwa ikimkabili ya kusafirisha dawa za kulevya.

Mahakama hiyo mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Zawadi Laizer, ilimuacha huru Mdude baada ya kusema, Jamhuri imeshindwa kuthibitisha tuhuma zilizokuwa zinamkabili.

Kada huyo wa Chadema amesota gerezani kwa siku 414, tangu Mei 2020, kwa shtaka la kusafirisha dawa za kulevya aina ya Heroin, zenye uzito wa gramu 23.4.

Mdude alikamatwa na Jeshi la Polisi mkoani Mbeya, tarehe 10 Mei 2021, baada ya kufanyiwa upekuzi katika hoteli moja jijini humo, alikokuwa amepanga, na kudaiwa kukutwa na dawa hizo.

Kongamano hilo, lililozinduliwa na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe.

Awali, baada ya msema chochote (MC) wa kongamano hilo, Twaha Mwaipaya kumkaribisha Mdude kuhutubia washiriki wake, walianza kuibuka kwa shangwe.

Na kuanza kucheza na Mdude wimbo wa dini wa Tumeuona Mkono wake Bwana ulioimbwa na kwaya ya Zabron Singers.

Wafuasi hao wa Chadema walitumia dakika kadhaa kucheza na Mdude, huku wengine wakimbeba juu kwa furaha.

Kufuatia tukio hilo, Mwaipaya aliwaomba wafuasi hao warudi katika nafasi zao, ili kumpa Mdude nafasi ya kuongea. Kisha baadae wataendelea kuserebuka naye.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataja mikakati ya kufikia trilioni 2 biashara Uturuki, Tz

Spread the loveWakati Tanzania na Uturuki zikidhamiria kuongeza kiwango cha biashara hadi...

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

error: Content is protected !!