March 6, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mdogo wa Lissu: Bunge limembagua Tundu

Tundu Lissu, Mbunge wa Singida Mashariki akiwa hospitali ya Nairobi

Spread the love

BUNGE la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linadaiwa kumbagua Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kwa kilichodaiwa ni kutokana na Spika wa bunge hilo, Job Ndugai kutofika Hospitali aliyolazwa Mbunge huyo au kutuma hata kiongozi wa bunge pamoja na kutopewa uangalizi akiwa kama mbunge. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Akizungumza na MwanaHALISI Online, Vincent Mughwai, mdogo wa Tundu Lissu amesema kuwa kama mwanafamilia amesikitishwa sana na hatua hiyo ya bunge ambalo ndio ofisi ya kaka yake.

Vincent amesema amesema kitendo hicho kimeibua hisia tofauti kwa wanafamilia kwani viongozi wote waliofika wamekwenda kwa vyeo vingine lakini kimsingi ofisi ya bunge ambayo ilipaswa kuwa mstari wa mbele kufahamu kila kinachoendelea haitoi ushirikiano.

“Licha ya Bunge kutangaza kuchangia Sh. 43 milioni kwa matibabu ya Lissu, baada ya malipo ya pesa hizo tu kukamilika Lissu hakupewa stahili zake nyingine kama mbunge aliyekuwepo kwenye matibabu kama walivyofanyiwa wengine,” amesema.

Amesema kuwa Bunge na Familia vilikaa vikao ambavyo havikuzaa muafaka wa kumsaidia Lissu ambapo walitaka familia iandike barua ya kuomba kutibiwa kwa ndugu pamoja na kuandika barua hiyo, hakuna majibu yoyote yaliyotolewa wala matibabu.

“Bunge na Serikali zilitoa tamko la kuchangia matibabu ya Lissu iwe ndani au nje ya nchi pamoja na kwamba hiyo ni haki yake lakini hadi sasa hilo halikufanyika,” amesema Vincent.

Fuatilia Mazungumzo haya kupiti Youtube Channel yetu ya MwanaHALISI TV .. Pia usisahau kusubscribe channel yetu ili kupata taarifa mbalimbali kwa haraka zaidi.

error: Content is protected !!