Monday , 30 January 2023
Home Kitengo Michezo Mdhamini Ligi Kuu bado kitendawili,
Michezo

Mdhamini Ligi Kuu bado kitendawili,

Almas Kasongo, Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi (TPLB)
Spread the love

 

ZIKIWA zimebaki siku 23 kabla ya Ligi Kuu Tanzana Bara kuanza kutimua vumbi kwa msimu mpya wa 2021/22, mpaka sasa mdhamini mpya bado hajawekwa wazi kufuatia kampuni ya Vodacom kujiondoa kwenye udhamini wa Ligi hiyo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Ligi hiyo ambayo kwa msimu huu itashikilisha timu 16, kutoka timu 20 kama ilivyokuwa kwenye misimu uliomalizika Julai Mwaka huu.

Katika kulitolea ufafanuzi jambo hilo, Mkurugenzi wa Bodi ya Ligi, Almas Kasongo, akizungumza kwenye semina ya waandishi wa habari iliyoandaliwa na bodi hiyo, Jumamosi ya tarehe 4 Septemba, 2021, alisema kmdhamini mpya atatajwa mapema kabla ya kuanza kwa ligi hiyo.

“Tunajua ligi inakwenda kuanza na kuhusu mdhamini mkuu, tutamtangaza hivi karibuni kabla ya msimu mpya wa kuanza,” alisema Kasongo.

Semina hiyo ilishirikisha jumla ya waandishi wa habari 100, kutoka vyombo mbalimbali nchini nzima katika kuwanoa na kujiweka sawa kwenye majukumu yao kabla ya kuanza kwa msimu mpya.

Ligi hiyo ambayo kwa msimu huu itaanza Septemba 29, baada ya kupigwa mchezo wa ngao ya jamii kati ya Simba na Yanga utakaochezwa Septemba 25, majira ya saa 11 jioni kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Katika hatua nyingine Kasongo hivi karibuni akihojiwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari aliweka wazi kuhusu ratiba ya Ligi Kuu kwa msimu wa 2021/22 na kusema kuwa itatoka mapema wiki hii.

“Ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara kwa msimu wa 2021/22, itatoka mapema wiki ijayo (wiki hii) ili timu ziweze kujiandaa,” alisema Kasongo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

GGML: Uwanja mpya wa Geita Gold FC kukamilika Mei, 2023

Spread the loveUWANJA wa Magogo unaojengwa na Halmashauri ya Mji wa Geita...

Michezo

Wanafunzi chuo Mwalimu Nyerere wapongezwa kwa ushindi

Spread the love  UONGOZI wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA)...

Michezo

Arsenal waipopoa Manchester United

Spread the loveKLABU ya Arsenal inayoshiriki Ligi Kuu England imewatandika Mashetani Wekundu...

Michezo

Mchezaji Singida apoteza maisha mazoezini

Spread the love  MCHEZAJI na kapteni wa timu ya vijana ya Singida...

error: Content is protected !!