May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mdee, wenzake wachongewa kwa Rais Samia

Catherine Ruge

Spread the love

 

UONGOZI wa Baraza la Wanawake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAWACHA), umemuomba Rais Samia Suluhu Hasani kuwafukuza wabunge waliopo bungeni bila kuwa na vyama. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Catherine Ruge, Mweka Hazina wa taasisi hiyo akizungumza na waandishi wa Habari leo tarehe 21 Aprili 2021, jijini Dodoma amesema, Rais Samia anakwenda kuzungumza bungeni huku kuwakiwa na ‘wabunge haramu.’

“Rais Samia anakwenda kuhutumia Bunge kwa mara ya kwanza tangu kuapishwa kwake kuwa rais, anatakiwa kutambua ndani ya Bunge kuna wabunge ambao hawastahili kuwepo ndani ya bunge.

“Kwa kuwa Rais Samia amekuwa akijipambanua na kueleza kuwa, utawala wake unazingatia kulinda na kuiheshimu Katiba ya Nchi, na alikula kuapo kwa kuhakikisha anaillinda Katiba basi, tunamuomba atambue kuwa ndani ya Bunge kuna watu 19 ambao hawana sifa ya kuwa wabunge,” amesema.

Wanachama waliofukuzwa na Chadema kwa kujipeleka wenyewe bungeni na kuapishwa kuwa wabunge wa Viti Maalum kinyume na umauzi wa chama hicho ni Halima Mdee, Grace Tendega, Esther Matiko, Cecilia Pareso, Esther Bulaya, Jesca Kishoa, Hawa Mwaifunga, Tunza Malapo, Naghenjwa Kaboyoka, Sophia Mwakagenda na Kunti Majala.

Wengine ni Anatropia Theonest, Salome Makamba na Conchesta Rwamlaza, Agnesta Kaiza, Nusrat Hanje, Asia Mohamed, Felister Njau na Stela Fiyao.

error: Content is protected !!