Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mdee, wenzake 18 wapigwa ‘kitanzi’
Habari za Siasa

Mdee, wenzake 18 wapigwa ‘kitanzi’

Spread the love

BARAZA la Wanawake la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Bawacha), limemtaka aliyekuwa mwenyekiti wake, Halima James Mdee na wenzake 18, “kuacha kutumia jina la baraza hilo,” kwa maslahi yao binafsi. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Makamu Mwenyekiti wa Bawacha-Zanzibar, Sharifa Suleiman amesema, Mdee na wenzake 18 waliofukuzwa uanachama wa chama hicho tarehe 27 Novemba 2020, bado wako katika mradi mahususi wa kuihujumu Chadema.

“Mdee na wenzake tuliowafukuza Chadema, bado wanaendelea kupanga hujuma dhidi ya Chadema kwa msaada wa watesi wetu,” imeeleza taarifa hiyo ya Sharifa anayekaimu mwenyekiti wa Bawacha  na kuongeza, “tunawaomba wanachama wetu, popote pale walipo, kuacha mara moja, kushirikiana na Mdee na wenzake.”

Sharifa ameeleza, kuwa Chadema kimepata taarifa kwamba Mdee na wenzake 18, wamepanga kufanya kongamano la wanawake kwa kutumia mgongo wa chama chake.

Amesema, “tumepata taarifa kuwa watu 19 waliofukuzwa uachama wa Chadema kwa makosa ya uasi, usaliti na hujuma dhidi ya chama na wapenda demokrasia, wanapanga mikakati yenye lengo la kutaka kujitafutia uhalali kutokana na haramu waliyoifanya.

https://www.youtube.com/watch?v=ul2rvkRZtk4

“Kwamba, watu hao wanashirikiana na mamlaka zilizochini ya watesi wetu na ambazo zinaendelea kuwalinda, kuandaa kitu wanachoita, ‘Kongamano la Wanawake.”

Anasema, “watu hao ambao kwa sasa siyo viongozi, wala siyo wanachama wa Chadema, kufuatia kuvuliwa uongozi na kufukuzwa uanachama na Kamati Kuu (CC), wanatumia nembo na jina la Chadema, kuwahadaa na kuwaghiribu wanawake.”

Mdee na wenzake 18, walifukuzwa uanachama wa Chadema, tarehe 27 Novemba 2020, baada ya kutuhumiwa kwa makosa mbalimbali, yakiwamo usaliti na kuhujumu chama; upendeleo na kujiteuwa kuwa wabunge na kisha kuapishwa, kinyume na maelekezo ya chama chenyewe.

Chadema kupitia vikao vyake vya kikatiba, viliweka msimamo wa pamoja wa kutopeleka wabunge wa Viti Maalum bungeni. Msimamo wa chama hicho, ulitokana na kile walichoita, “uchaguzi ulioleta viti maalum, uliendeshwa kinyume na sheria za uchaguzi.”

Wengine waliofutwa uwanachama, ni aliyekuwa mbunge wa Bunda Mjini, Ester Bulaya na mwezake wa Tarime Mjini, Esther Matiko; aliyekuwa katibu mkuu wa Baraza la Vijana la chama hicho (Bavicha), Nusrat Hanje na Katibu Mkuu wa Bawacha, Grace Tendega.

Wengine, ni aliyekuwa Makamu Mwenyekiti Bawacha (Bara), Hawa Mwaifunga; Naibu Katibu Mkuu Bawacha (Bara), Jesca Kishoa; Katibu Uenezi Bawacha, Agnesta Lambat; mwenyekiti wa Chadema mkoani Mtwara, Tunza Malapo na naibu katibu mkuu wa Bawacha Zanzibar, Asia Mohamed.

Wamo pia,  Ceciia Pareso, Naghenjwa Kaboyoka, Sophia Mwakagenda, Kunti Majala, Salome Makamba,  Anatropia Theonest, Conchesta Lwamlaza, Felister Njau na Stella Siyao.

Wanachama hao, waliopachikwa jina la ‘Covid 19’, mbali na kuvuliwa uongozi na kufukuzwa uanachama, wamepigwa marufuku kutumia jina la Chadema, kwa jambo lolote lile ambalo watalifanya binafsi; na au katika jamii.

Akizungumzia hilo, Sharifa amesema, chama hicho, hakitasita kuwachukulia hatua kali, wanachama wake watakaoshirikiana na genge hilo, bila kuangalia sura na nafasi zao ndani ya chama.

Amesema, “Mdee na wenzake, siyo wanachama wa Chadema. Hivyo basi, kila atakayeshirikiana naye, atambue atakuwa anakiuka taratibu na maamuzi ya chama na kwa msingi huo, atachukuliwa hatua stahiki kwa mujibu wa katiba ya chama na mwongozo wa Bawacha.”

Sharifa amesema, Bawacha haijandaa kongamano lolote la wanawake na kuwataka wanachama wake wawe na uvumilifu wakati uongozi wa baraza hilo likiandaa taratibu za kujaza nafasi za viongozi waliofukuzwa.

“Tuendelee kuwataka wanawake wote wa Bawacha na Chadema kwa ujumla, wakati tukiendelea kujipanga kwa ajili ya kutekeleza maazimio ya Kamati Kuu, ikiwa ni pamoja na kuziba nafasi za waliofukuzwa.

“Naomba tuzidi kuwa imara, kama jadi yetu, kwa kusimama na chama chetu, pia kufahamishana kuwa uamuzi wa kuwafukuza uanachama Mdee na wenzake 18, unaendelea kutamalaki na kutekelezwa, na bado haujabadilika,” amesisitiza.

Kaimu Makamu mwenyekiti huyo wa Bawacha amesema, baraza hilo litaendelea kufuatilia nyendo zao ili kuchukua hatua za haraka kudhibiti vitendo hivyo na vingine ambavyo vitajitokeza.

“Mbali ya kuendelea kufuatilia nyendo zao na kuzichukulia hatua za haraka kwa lengo la kuzuia matumizi mabaya ya nembo za Bawacha na Chadema, ikiwa ni mwendeleo wa uhalifu dhidi ya taratibu za kisheria zinazohusu chama na nchi, Chadema bado kinaendelea kuamini kuwa Mdee na wenzake, ni wasaliti wa haki nchini na hivyo, hawastahili kuhurumiwa.”

Kwa mujibu wa taarifa ambazo MwanaHALISI Online imezipata, mchakato wa kutengeneza uasi ndani ya Chadema, uliratibiwa kwa ukamilifu na Mdee, Bulaya, Tendeka, Agnesta na Kunti.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, wanachama hao, walifanya kazi hiyo kwa takribani wiki tatu, kwa msaada wa baadhi ya makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambao walikuwa viongozi wakuu wa Chadema.

Ni Tendega, aliyewasilisha majina Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kupitia kwa Kunti, Mdee na Agnesta, huku utetezi mkuu ukiwa viti maalum ni mali ya wanawake na hivyo, ni makosa kwa chama kuwaingilia.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!