Saturday , 10 June 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Mdee na wenzake wajisalimisha kwa msajili
Habari za SiasaTangulizi

Mdee na wenzake wajisalimisha kwa msajili

Spread the love

 

ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Halima Mdee na wenzake 18, wametinga katika Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, kupinga kutimuliwa ndani ya chama hicho. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Mdee na wenzake walitimuliwa Chadema tarehe 27 Novemba 2020, kwa kosa la usaliti kufuatia hatua yao ya kukubali kuapishwa kuwa wabunge viti maalumu, kinyume na msimamo wa chama hicho kutopeleka wawakilishi bungeni.

Tarehe 24 Novemba mwaka jana, Mdee na wenzake waliapishwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai, kuwa wabunge viti maalumu kwa mgongo wa Chadema.

Akizungumza na MwanaHALISI Online kwa simu, leo tarehe 14 Julai 2021, Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa, Sixty Nyahoza, amesema wabunge hao wamefikisha malalamiko katika ofisi hiyo, wakipinga uamuzi wa Chadema kuwafukuza.

Sisty Nyahoza, Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Tanzania

Nyahoza amesema baada ya kupokea malalamiko hayo, ofisi hiyo iliiandikia barua Chadema, ili wajieleze kufuatia malalamiko hayo.

“Tumepokea malalamiko kutoka kwa wabunge wote 19, sisi hatuingilii maamuzi ya vyama ila tunatekeleza wajibu wetu wa kusimamia Sheria ya Vyama vya Siasa. Ndiyo maana tukawaambia wawasilishe maelezo,” amesema Nyahoza.

Mbali na Mdee, wengine waliotinga kwa msajili wa vyama vya siasa kupinga kutimuliwa Chadema ni, waliokuwa viongozi wa Bawacha, Hawa Mwaifunga (Makamu Mwenyekiti). Grace Tendega (Katibu Mkuu). Jesca Kishoa (Naibu Katibu Mkuu) na Agnesta Lambart (Katibu Mwenezi).

Wengine ni, waliokuwa wajumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Ester Bulaya na Esther Matiko, pamoja na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Mtwara, Tunza Malapo.

Pamoja na Cecilia Pareso, Asia Mwadin Mohamed, Felister Njau, Naghenjwa Kaboyoka, Sophia Mwakagenda, Kunti Majala, Stella Siyao, Salome Makamba, Anatropita Theonest na Conchesta Lwamlaza.

Benson Kigaila, Naibu Katibu Mkuu Chadema Bara

Awali, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Bara, Benson Kigaila, alisema wamepokea barua kutoka kwa Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, akiwataka wajieleze kuhusu uamuzi wao wa kuwafukuza wabunge hao.

Kigaila alisema barua hiyo iliandikwa tarehe 6 Julai 2021 na kwamba chama hicho kimewasilisha maelezo yao kwa msajili wa vyama vya siasa, tarehe 9 Julai mwaka huu.

Chadema kiligoma kuwatambua kina Mdee na wenzake, kwa maelezo kwamba walienda bungeni kupitia mlango wa nyuma.

Chama hicho kiliweka msimamo wa kutopeleka wawakilishi wake bungeni, kikipinga matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka jana, kwa madai kwamba mchakato wake haukuwa huru na wa haki.

Hata hivyo, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), mara kadhaa imekanusha madai hayo ikisema kwamba iliendesha uchaguzi huo kwa haki.

Kwa mujibu wa matokeo ya uchaguzi huo yaliyotangazwa na NEC, Chama Cha Mapinduzi kilishinda uchaguzi wa wabunge na madiwani kwa zaidi ya asilimia 90.

Kwa sasa CCM kina wabunge zaidi ya 300, huku vyama vya upinzani vikiwa na wabunge sita wa majimbo, ACT-Wazalendo wanne, Chama cha Wananchi (CUF) mmoja na Chadema mmoja.

Pamoja na wabunge viti maalumu 19, ambao wamefukuzwa Chadema.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

MichezoTangulizi

Benki ya NBC yakabidhi kombe la ubingwa wa ligi kuu kwa Yanga

Spread the loveMDHAMINI Mkuu wa ligi ya NBC, Benki ya Taifa ya...

BiasharaTangulizi

TLS wajitosa sakata la ukodishaji wa bandari

Spread the love  CHAMA cha wanasheria Tanzania (TLS), kimejitosa katika sakata la...

BiasharaTangulizi

Ngoma bado mbichi mkataba wa Bandari

Spread the love  SAKATA la mkataba wa uendeshaji, uendelezaji na uboreshaji wa...

BiasharaTangulizi

Mkurugenzi TPA: Mkataba unaweza kuvunjwa

Spread the loveMKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA),...

error: Content is protected !!