Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mdee, Mch. Msigwa wataka ripoti ya Corona ijadiliwe bungeni
Habari za Siasa

Mdee, Mch. Msigwa wataka ripoti ya Corona ijadiliwe bungeni

Bunge la Tanzania
Spread the love

WABUNGE wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wameitaka serikali kuwasilisha bungeni  ripoti ya tathimini ya ugonjwa wa Homa Kali ya Mapafu, inayosabishwa na Virusi vya Corona (COVID-19). Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Halima Mdee, Mbunge wa Kawe na Mchungaji Peter Msigwa, Mbunge wa Iringa Mjini, wametoa hoja hiyo leo tarehe 31 Machi 2020 bungeni jijini Dodoma.

Katika hoja yake, Mdee ameitaka serikali kuwasilisha ripoti hiyo ili wabunge waijadili kwa lengo la kuandaa mpango wa dharula na bajeti, kwa ajili ya kukabiliana na ugonjwa huo.

“Katika kipindi hiki nilidhani ni busara serikali kupitia Wizara ya Afya, itoe taarifa ya kina bungeni kuhusu suala la Corona. Tanzania hali ikoje na hatua zilizochukuliwa. Nilidhani muhimu hili suala kulijadili ili tujue serikali ina mpango gani wa kidharula na kibajeti.

Kama nchi nyingine zinavyofanya, serikali inafidia wananchi na wafanyabiashara ili waweze kutulia nyumbani, hili suala ni muhimu,” amesema Mdee.

Wakati huo huo, Mdee ameshauri uongozi wa bunge kuhakikisha inawapima wabunge wote ili kujua kama kuna walioambukizwa ugonjwa wa COVID-19, kwa ajili ya kuzuia wasiambukize wengine.

“Labda tungepimwa ili ijulikane Halima nina corona, tupimwe wote tukigundua tuko salama tuje tujadiliane, hili ni bunge la mwisho. Nakuomba sana kuchukua hatua,” ameshauri Mdee.

Mchungaji Msigwa, ameungana na hoja ya Mdee, na kuitaka serikali iwasilishe bungeni ripoti hiyo, kwa ajili ya kupanga mikakati ya kujinasua na janga hilo, hasa katika kuhakikisha wananchi wanakuwa salama na uchumi wa nchi hauyumbi.

“Tusipokuwa waangalifu, tunaweza kudondosha mmoja mmoja, tunaweza kukaa mbali lakini nyumbani hali ni ngumu, napenda kuungana na hoja ya Halima, nataka tujadilliane kama wabunge, si suala la ugonjwa tu, lakini kiuchumi tumeathirika, serikali itueleze na ije na mpango. Kwa pamoja tushirikiane njia gani tutapita ili kukwamuana na tatizo hilo,” amesema Mch. Msigwa.

Akijibu hoja hizo, Spika Job Ndugai amesema bunge linazifanyia kazi na kueleza kwamba kuanzia kesho wabunge watajadili suala hilo katika hotuba ya waziri mkuu.

“Wote mmeongea kitu kile kile na msisitizo wenu tujadiliane na ndio maana ya bunge, na bahati nzuri sisi ndio wakailishi wa wananchi. Kazi yetu kuwawakilisha, mkutano wetu ndiyo fursa ya kujadiliana, kwenye vita hii lazima tuwe wamoja, na kila mmoja atakuwa makini kusikiliza na kuchukua hatua,” amejibu Spika Ndugai na kuongeza:

“Kwa hiyo niwatie moyo wabunge wote, bahati nzuri kesho tunaanza hotuba ya waziri mkuu, ofisi ambayo inaratibu mambo yote haya. Sababu corona ni mtambuka inahusu wizara zote.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Bajeti ya Ikulu 2024/25 kuongezeka, bunge laombwa kurudhia Sh. 1.1 trilioni

Spread the love  WIZARA ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa...

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

error: Content is protected !!