Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mdee, Bulaya, Jacob wabebeshwa tuhuma saba
Habari za SiasaTangulizi

Mdee, Bulaya, Jacob wabebeshwa tuhuma saba

Spread the love

JUMLA ya viongozi na wafuasi 27 wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wamepandishwa kizimbani wakituhumiwa kutenda makossa saba. Anaripoti Hamis Mguta, Dar es Salaam … (endelea).

Watuhumiwa hao wamepandishwa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam wakidaiwa kufanya mkusanyiko na kutotii amri halali katika geti la gereza la Segerea.

Leo tarehe 23 Machi 2020, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi, washtakiwa 15 kati ya 27, wamesomewa mashtaka yao.

Miongoni mwa viongozi hao ni pamoja na Halima Mdee, Mbunge wa Kawe; Ester Bulaya, Mbunge wa Bunda Mjini; Boniface Jacob, Meya wa Manispaa ya Ubungo na Patrick Assenga, Diwani wa Tabata.

Shtaka la kwanza limesomwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Renatus Mkude ambalo ni kutotii amri halali, washtakiwa wote wamedaiwa tarehe 13 Machi 2020 , eneo la gereza la Segerea, Ilala jijini Dar es Salaam kwa makusudi, waligomea amri halali iliyotolewa na askari mwenye namba P3648, Sajenti John ambaye ni mlinzi wa geti la gereza hilo.

Shtaka la Pili limesomwa na wakili wa Serikali, Mkunde Mshana ambalo ni kufanya kusanyiko lisilohalali linalowakabili watuhumiwa wote, inadaiwa tarehe 13 Machi, 2020 walikusanyika kwenye geti la gereza la Segerea visivyohalali na kusababisha hali isiyo ya kawaidi iliyopelekea hofu.

Shtaka la tatu linawakabili watuhumiwa ambapo inadaiwa, tarehe 13 Machi 2020, wanadaiwa kufanya uharibifu kwenye geti la gereza la Segerea ambalo ni mali ya serikali ya Jamhuri.

Shtaka la nne limesomwa na Wakili wa Serikali, Ester Martin ambapo linamkabili Mdee la kutoa lugha yenye kuudhi, inadaiwa tarehe 13 Machi 2020 alitoa maneno ‘msenge, vibaraka wa CCM, mnakaa nyumba za bati, mishahara yenye elfu 70,  wewe Sajenti fungua geti.’

Shitaka la tano linamkabili Bulaya ambapo inadaiwa, tarehe 13 Machi 2020, anadaiwa kutoa lugha ya kuudhi ‘(tusi), vibaraka wa CCM, mnakaa nyumba za bati, mishahara yenye elfu 70, wewe Sajenti fungua geti wakimwambia Sajenti John.’

Shtaka la sita linamkabili Jacob la kutoa maneno ya kuudhi kwa Sajenti John, anadaiwa kutenda tarehe 13 Machi 2020 na kwamba alitoa maneno “wewe (tusi) acha kugombana na wanawake, gombana na mimi na mwanaume ….”.

Shtaka la saba linamkabili Jacob la shambulio ambapo anadaiwa tarehe 13 Machi 2020, akiwa kwenye gereza la Segerea alimshambulia kwa kumfunga Sajente John, na kusababisha kumchania shati lake akiwa anatekeleza majukumu ya ulinzi kwenye geti la ngome ya Segere.

Washtakiwa wamekana mashtaka hayo. Upande wa serikali umedai kuwa, umekamilisha upelelezi na wameiomba mahakama kupanga terehe kwa ajili ya usikilizwaji wa awali.

Washtakiwa wamedhaminiwa kwa mdhamini mmoja kila mmoja aliyesaini bondi ya shilingi 4 milioni. Kesi imeahirishwa hadi tarehe 23 Aprili 2020.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!