April 13, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mdee atoka mahabusu

Spread the love

JESHI la Polisi mkoani Kagera, limemwacha kwa dhamana Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake la Chadema (Bawacha), Halima Mdee. Anaripoti Hamis Mguta … (endelea).

Jeshi hilo lilimshikilia Mdee ambaye pia ni Mbunge wa Kawe, tangu jana tarehe 14 Julai 2019, kwa tuhuma za kufanya uchochezi.

Mdee, Grace Tendega, Katibu wa Bawacha; Conchesta Rwamlaza, Mwenyekiti wa Bawacha Mkoa wa Kagera na Anatropia Theonest; Mbunge Viti Maalum jana walikamatwa na kuhojiwa ambapo Mdee pekee hakupewa dhamana.

Awali, Polisi waligoma kumpa dhamana Mdee wakidai wanasubiri maelekezo kutoka kwa Kamanda wa Mkoa wa Kagera, aliyekuwa kwenye ziara ya Rais John Magufuli.

Taarifa iliyotolewa Chadema imeeleza kuwa, Mdee amedhaminiwa na watu wawili ambapo pia ametakiwa kuripoti kituoni hapo baada ya mwezi mmoja au wakati wowote polisi watakapomuhitaji.

error: Content is protected !!