Friday , 3 February 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Mdee ataka sensa ibaini maeneo yasiyokuwa na maji
Habari za Siasa

Mdee ataka sensa ibaini maeneo yasiyokuwa na maji

Halima Mdee
Spread the love

 

MBUNGE Viti Maalumu (asiye na chama bungeni), Halima Mdee, ameishauri Serikali itumie sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika 2022, kubaini hali ya upatikanaji maji, hasa maeneo ya vijijini. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Mdee ametoa ushauri huo leo Jumanne, tarehe 29 Juni 2021, katika kipindi cha maswali na majibu bungeni jijini Dodoma.

Mbunge huyo wa viti maalumu, amesema takwimu za hali ya upatikanaji maji zilizopo sasa, haziendani na hali halisi ya upatikanaji huduma hiyo, hasa katika maeneo ya vijijini.

“Takwimu za Serikali zinaoensha kwamba maji vijijini yanapatikana kwa asilimia 74 na mijini asilimia 85 kwenda 90, lakini uhalisia unaonesha kwamba watu wanapata maji kutokana na kuweka miundombinu na siyo nyumba kwa nyumba,” amesema Mdee na kuongeza:

“Sasa kwa kuwa sasa hivi tunaenda kwenye sensa ya Taifa, ambapo watu wataenda kufanyiwa hesabu nyumba kwa nyumba. Kwa nini msitumie utaratibu huu wa sensa ili kuweza kupata takwimu halisi ya kila nyumba inayopata maji katika nchi hii.”

Akijibu ombi hilo, Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, amesema wizara hiyo imeshaanza kufanya utafiti ili kubaini vijiji vilivyokosa maji.

“Wizara ya maji inafanya mageuzi makubwa sana na eneo unalozungumzia tumelifanyia kazi, tumekutana na watu wetu wa takwimu kuhakikisha kwamba tunakwenda kwenye hilo suala,” amesema Aweso

“Lakini tunataka tujiongeze mbali zaidi, badala ya kusema tuna asilimia ngapi watu wanapata maji, tunataka tujue Tanzania kuna vijiji vingapi vimepata maji, vingapi havijapa maji ili tuhakikishe tunaviongezea nguvu hasa maeneo ambayo hayana maji ili tupate maji safi na salama.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Kamati ya Bunge yaitaka Serikali kuchunguza dawa za asili

Spread the love  KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo...

Habari za Siasa

Kada NCCR-Mageuzi aliyepotea aokotwa porini akiwa taabani, hajitambua

Spread the love  MWENYEKITI wa Jumuiya ya Vijana ya Chama cha NCCR-Mageuzi,...

Habari za Siasa

ACT Wazalendo yataka Jaji Mkuu, Jaji Biswalo wajiuzulu kupisha uchunguzi fedha za Plea Bargaining

Spread the love  CHAMA cha ACT-Wazalendo, kimemtaka Jaji wa Mkuu wa Tanzania,...

Habari za Siasa

Kigogo ACT-Wazalendo: Vyama vya upinzani vilikosea kumpokea Membe, Lowassa

Spread the love  KATIBU Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Ado Shaibu, amesema...

error: Content is protected !!