February 27, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mdalasini tiba magonjwa mbalimbali ya binadamu

Spread the love

IMEELEZWA kuwa mimea ya mchai chai pamoja na Mdalasini inasaidia kutibu magonjwa mbalimbali ya binadamu, anaandika Dany Tibason.

Hayo yameelezwa leo bungeni na Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, William Ole Nasha alipokuwa akijibu swali la mbunge wa Viti Maalum, Maida Hamad Abdallah (CCM).

Akiuliza swali la nyongeza mbunge huyo alitaka kujua ni kwanini serikali ina kiwanda kimoja cha kuzalisha bidhaa ya Mdalasini na Mchai Chai wakati ina kazi muhimu kwa binadamu.

Awali katika swali la msingi Maida, alitaka kujua kama serikali ina mkakati wowote wa kutoa elimu kwa wakulima wa mazao ya Mdalasini na Mchai Chai ili kufahamu faida ya mazao hayo ili kuweza kuongeza uzalishaji.

Akijibu maswali hayo Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Umwagiliaji William Ole Nasha alisema mazao hayo yanazalsihwa kwa wingi na wakulima wadogo hususani katika mikoa ya Tanga, Morogoro na Kigoma.

“Kutokana na kuongezeka kwa mahitaji ya mazao hayo na faida za kitabibu na kiburudisho kumechochea ongezeko la bei na hivyo kuleta hamasa kwa wakulima.

error: Content is protected !!